Watu hawa ni kama madoa machafu miongoni mwenu, wanawatia aibu mnapokutanika pamoja kuonesha upendo miongoni mwenu na kula chakula kwa pamoja kama kanisa. Pasipo kuwa na aibu wanakula pamoja nanyi. Wanajijali wao wenyewe tu. Wao ni kama mawingu yasiyo na mvua yanayosukumwa na upepo kila upande. Wako kama miti isiyo na matunda wakati wa mavuno ambayo hung'olewa kutoka ardhini. Hivyo wamekufa mara mbili.
Watu hawa ni madoa katika karamu zenu za ushirika. Wanak ula nanyi bila kuwa na kiasi, wakicheka na kujishibisha na kunywa bila kujali wengine. Wao ni kama mawingu yanayochukuliwa na upepo huku na huku pasipo kuleta mvua; ni kama miti ya kiangazi iliy opukutika bila kuwa na matunda, ambayo imekufa kabisa na kung’olewa pamoja na mizizi yake.