Yohana 6:35-71
Neno: Bibilia Takatifu
35 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima. Ye yote ajaye kwangu hataona njaa kamwe, na ye yote aniaminiye, hataona kiu kamwe. 36 Lakini kama nilivyokwisha waambia, mnaniona lakini bado hamtaki kuamini. 37 Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe. 38 Kwa maana sikushuka kutoka mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu, bali nitimize mapenzi yake yeye aliyenituma. 39 Na mapenzi yake yeye aliyenituma ni haya: kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa bali niwafufue wote siku ya mwisho. 40 Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni haya: wote wamwonao Mwana na kumwamini wawe na uzima wa milele. Nami nitawafufua siku ya mwisho.”
41 Wayahudi wakaanza kunung’unika kwa kuwa alisema: “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 42 Wakasema, “Huyu si Yesu mwana wa Yusufu? Na baba yake na mama yake si tunawajua? Anawezaje basi kutuambia kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”
43 Lakini Yesu akawaambia, “Acheni kunung’unika. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama Baba aliyenituma hakumvuta kwangu; nami nitamfufua siku ya mwisho. 45 Kama manabii walivyoandika, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Ye yote amsikilizaye Baba na kuji funza kutoka kwake, huja kwangu. 46 Hii haina maana kwamba kuna mtu aliyekwisha kumwona Baba. Ni yule aliyetoka kwa Mungu peke yake, ndiye aliyekwisha kumwona Baba. 47 Nawaambieni kweli: anayeamini anao uzima wa milele. 48 Mimi ni mkate wa uzima. 49 Baba zenu walikula mana jangwani, wakafa. 50 Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51 Mimi ni mkate wa uzima uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu ataishi milele. Na mkate wenyewe ni mwili wangu ambao nitautoa ili watu wote ulimwenguni wapate kuishi milele.”
52 Hapo Wayahudi wakaanza kubishana kwa hasira wakiulizana, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”
53 Kwa hiyo Yesu akasema, “Ninawaambieni hakika, msipoula mwili wangu mimi Mwana wa Adamu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. 54 Mtu ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula halisi na damu yangu ni kinywaji halisi. 56 Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anaishi ndani yangu na mimi ninaishi ndani yake. 57 Kama vile Baba wa uzima alivyonituma, na kama nipatavyo uzima kutoka kwake, kadhalika, ye yote anilaye ataishi kwa sababu yangu. 58 Huu ndio mkate uliotoka mbinguni, si kama ule mkate walio kula baba zenu hatimaye wakafa. Alaye mkate huu ataishi milele.” 59 Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sina gogi huko Kapernaumu.
Wafuasi Wengi Wamwacha Yesu
60 Wengi wa wanafunzi wake waliosikia maneno haya walisema, “Mafundisho haya ni magumu! Ni nani awezaye kukubaliana nayo?”
61 Yesu alitambua kwamba wafuasi wake walikuwa wakilalamika kuhusu mafundisho yake. Kwa hiyo akawauliza, “Mafundisho haya yanawaudhi? 62 Ingekuwaje basi, kama mngeniona mimi Mwana wa Adamu nikirudi mbinguni nilikotoka? 63 Roho wa Mungu ndiye anayetoa uzima, uwezo wa mwanadamu haufai kitu. Maneno haya ni Roho na ni uzima. 64 Lakini baadhi yenu hamuamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini na yule ambaye angemsaliti. 65 Akaendelea kusema, “Ndio sababu nili waambia kwamba hakuna awezaye kuja kwangu kama Baba hakumwe zesha.”
66 Tangu wakati huo wanafunzi wake wengi waliondoka wakaacha kumfuata. 67 Yesu akawauliza wale wanafunzi kumi na wawili, “Ninyi pia mnataka kuondoka?” 68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. 69 Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiye Mtakatifu wa Mungu.”
Mungu.”
70 Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni shetani!” 71 Hapa alikuwa anamsema Yuda, mwana wa Simoni Iskariote ambaye, ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, baadaye angemsaliti Yesu.
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica