Yohana 20
Neno: Bibilia Takatifu
Kaburi Tupu
20 Jumapili asubuhi na mapema, kukiwa bado giza, Mariamu Mag dalena alifika kaburini akakuta lile jiwe lililokuwa limeziba mlango wa kaburi limeondolewa. 2 Kwa hiyo akaenda mbio kwa Simoni Petro na yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akawaambia, “Wameu chukua mwili wa Bwana kutoka mle kaburini na hatujui wameuweka wapi!” 3 Petro na yule mwanafunzi wakaondoka mara kuelekea kabu rini. 4 Wote wawili walikuwa wanakimbia lakini yule mwanafunzi akakimbia mbio zaidi kuliko Petro, akawahi kufika kaburini. 5 Alipofika akainama na kuchungulia mle kaburini akaona ile sanda, lakini hakuingia ndani. 6 Ndipo Petro akaja akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani ya kaburi. Naye akaona ile sanda 7 na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu kimekunjwa na kuwekwa kando ya ile sanda. 8 Kisha yule mwanafunzi aliyewahi kufika kaburini naye akaingia ndani; akaona, akaamini. 9 Kwa maana mpaka wakati huo walikuwa bado hawajaelewa yale Maandiko yaliyotabiri kuwa angefufuka kutoka kwa wafu. 10 Wale wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao.
Yesu Anamtokea Mariamu
11 Lakini Mariamu akakaa nje ya kaburi akilia. Na alipokuwa akilia akainama kutazama mle kaburini. 12 Akaona malaika wawili wamevaa nguo nyeupe, wamekaa pale mwili wa Yesu ulipokuwa, mmoja upande wa miguuni na mwingine upande wa kichwani! 13 Wakamwuliza Mariamu, “Mama, mbona unalia?” Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui wamemweka wapi.” 14 Alipokuwa akisema haya akageuka, akamwona Yesu amesimama nyuma yake, lakini hakumtambua! 15 Yesu akamwambia, “Mama, mbona unalia? Unamta futa nani?” Mariamu alidhani aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akajibu, “Kama ni wewe umemchukua tafadhali nionyeshe ulipomweka ili nimchukue.” 16 Yesu akamwita, “Mar iamu.” Ndipo Mariamu akamgeukia Yesu, akamwambia kwa Kiebrania, “Rabboni!’ 17 Yesu akamwambia, “Usin ishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.” 18 Kwa hiyo Mariamu Magdalena akaenda akawakuta wanafunzi akawaambia, “Nimemwona Bwana!”
Yesu Anawatokea Wanafunzi Wake
19 Jumapili hiyo jioni, wakati wanafunzi walikuwa pamoja huku milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwato kea! Akasimama kati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 20 Baada ya kusema haya, aliwaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi walifurahi sana walipomwona Bwana! 21 Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama Baba alivyonituma, mimi pia nawatuma ninyi.” 22 Na alipokwisha kusema haya akawavuvia pumzi yake akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Mkimsamehe mtu ye yote dhambi zake, atakuwa amesamehewa. Msipomsamehe, atakuwa hajasame hewa.”
Yesu Anamtokea Tomaso
24 Tomaso, aliyeitwa Pacha, hakuwepo wakati Yesu aliwatokea wanafunzi wenzake. 25 Kwa hiyo wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Lakini yeye akawaambia, “Sitaamini mpaka nione alama za misumari katika mikono yake na niguse kwa vidole vyangu makovu ya misumari na kuweka mkono wangu ubavuni mwake.”
26 Siku nane baada ya haya, wanafunzi walikuwa pamoja tena katika chumba kimoja na Tomaso pia alikuwepo. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akawatokea akasimama kati yao akawaambia, “Amani iwe nanyi.” 27 Ndipo akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa; tazama mikono yangu halafu nyoosha mkono wako uguse ubavu wangu. Usiwe na mashaka bali uamini.” 28 Tomaso akasema, “Bwana wangu na Mungu wangu!” 29 Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”
30 Yesu alifanya ishara nyingine nyingi mbele za wanafunzi wake ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki. 31 Lakini hizi zimeandikwa ili muweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.
Copyright © 1989 by Biblica