Warumi 2
Neno: Bibilia Takatifu
Hukumu Ya Mungu
2 Kwa hiyo huna udhuru wo wote, hata ukiwa nani, unapowahu kumu wengine. Kwa maana unapowahukumu wengine unajihukumu mwe nyewe, kwa kuwa wewe uliye hakimu unafanya mambo hayo hayo. 2 Tunajua kwamba hukumu ya Mungu huwafikia kwa halali wote wanaotenda mambo haya. 3 Je, wewe uliye binadamu tu, unapowahuku mu watu wanaofanya mambo hayo na huku wewe mwenyewe pia unafanya hayo hayo, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? 4 Au labda unad harau wingi wa huruma, uvumilivu na subira ya Mungu, ukasahau kwamba wema wake una shabaha ya kukufanya utubu?
5 Lakini kwa sababu ya ugumu na ukaidi wa moyo wako usioku bali kutubu, unajiwekea ghadhabu kwa siku ile ambapo ghadhabu ya Mungu na hukumu yake ya haki itadhihirishwa. 6 Siku hiyo, Mungu atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake. 7 Wale ambao hutenda wema wakati wote na kutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyo haribika, Mungu atawapa uzima wa milele. 8 Lakini wote watafu tao kujinufaisha, wanaokataa kweli na kufuatauovu, watapokea ghadhabu na hasira ya Mungu. 9 Kwa maana kila binadamu atendaye uovu atapata mateso na shida, kuanzia kwa Myahudi na kisha kwa mtu wa mataifa mengine. 10 Lakini Mungu atawapa utukufu, heshima na amani wote watendao mema; Wayahudi kwanza na kisha watu wa mataifa mengine. 11 Kwa maana Mungu hana upendeleo.
12 Watu wote waliotenda dhambi pasipokuwa na sheria ya Musa wataangamia pasipo sheria; na wale wote waliotenda dhambi chini ya sheria ya Musa watahukumiwa kwa sheria iyo hiyo. 13 Kwa maana wanaohesabiwa haki mbele ya Mungu si wale wanaosikia bali ni wal ewanaotii maagizo ya sheria. 14 Watu wa mataifa mengine ambao hawana sheria ya Musa, wanapoamua kutenda yale ambayo yameagizwa na sheria kwa kuongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa wamejiwekea sheria, ingawa hawana sheria ya Musa. 15 Kwa jinsi hii matendo yao yanaonyesha kwamba yale yaliyoagizwa katika she ria ya Musa yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia hush uhudia hivyo; kwa maana mawazo yao mara nyingine huwashtaki na mara nyingine huwatetea. 16 Kwa hiyo, kama Habari Njema ninay ohubiri inavyosema, hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile ambayo Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo, atayahukumu mawazo ya siri ya wanadamu.
Wayahudi Na Sheria Ya Musa
17 Na wewe je? Wewe unayejiita Myahudi: unaitegemea sheria ya Musa na kujisifia uhusiano wako na Mungu; 18 unajua mapenzi ya Mungu na unatambua lililo bora kutokana na hiyo sheria. 19 Kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu na mwanga kwa wale walioko gizani; 20 mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa watoto wachanga, kwa kuwa una hakika kwamba ndani ya hiyo sheria mna maarifa na kweli yote: 21 wewe unayewafundisha wengine, mbona hujifunzi mwenyewe? Wewe unayehubiri kwamba watu wasiibe, wewe huibi? 22 Wewe unayewaambia watu wasizini, wewe huzini? Wewe uchukiaye miungu ya sanamu, huibi katika mahekalu? 23 Wewe unayejisifia sheria, humwaibishi Mungu kwa kuvunja sheria? 24 Kwa maana Maandiko yanasema, “Kwa ajili yenu ninyi Wayahudi, jina la Mungu linatukanwa miongoni mwa mataifa ya watu wasiom jua Mungu.”
25 Kutahiriwa kuna thamani tu iwapo unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, umekuwa kama hukutahiriwa. 26 Kwa hiyo kama watu ambao hawakutahiriwa wanatimiza maagizo ya she ria, je, Mungu hatawahesabu kuwa kama waliotahiriwa? 27 Ndipo wale ambao kimwili hawakutahiriwa lakini wanatii sheria watawa hukumu ninyi mlio na Maandiko ya sheria nakutahiriwa lakini mna vunja sheria. 28 Kwamaana Myahudi wa kweli si yule anayeonekana kwa dalili za nje, wala tohara ya kweli si kitu cha kimwili. 29 Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ya kweli ni jambo la moyoni, jambo la kiroho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa jinsi hii anapata sifa kutoka kwa Mungu, wala si kutoka kwa wanadamu.
Copyright © 1989 by Biblica