Waefeso 4:22-32
Neno: Bibilia Takatifu
22 Vueni maisha yenu ya zamani muweke kando hali yenu ya asili ambayo huharibiwa na tamaa potovu. 23 Nia zenu zifanywe upya 24 na mvae utu upya ulioumbwa kwa mfano wa Mungu katika haki na utakatifu. 25 Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja. 26 Mkikasirika, msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima 27 na kumpa she tani nafasi. 28 Mwizi asiibe tena, bali afanye kazi halali kwa mikono yake ili aweze kuwa na kitu cha kuwapa wenye kuhitaji msaada. 29 Msiruhusu maneno machafu yatoke vinywani mwenu, bali mazungumzo yenu yawe ya msaada katika kuwajenga wengine kufuatana na mahitaji yao, ili wale wanaowasikiliza wapate kufaidika. 30 Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi. 31 Ondoeni kabisa chuki yote, ghadhabu, hasira, ugomvi na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. 32 Muwe wema na wenye mioyo ya upendo kati yenu, na kusameheana kama Mungu alivyowasamehe kwa ajili ya Kristo. Watoto Wa Nuru
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica