Ufunua wa Yohana 9
Neno: Bibilia Takatifu
Tarumbeta Ya Tano
9 Kisha malaika wa tano akapiga tarumbeta yake, nikaona nyota iliyokuwa imeanguka kutoka angani hadi ardhini. Nyota hiyo ili pewa ufunguo wa shimo la kuzimu. 2 Alipolifungua hilo shimo, moshi ulitoka ndani yake kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vilitiwa giza kwa ajili ya ule moshi uliotoka katika shimo hilo. 3 Kisha, katika ule moshi wakatoka nzige wakatua ardhini. Nao wakapewa nguvu kama nguvu ya nge wa duniani. 4 Waliambiwa wasidhuru nyasi za nchi, wala majani, wala mmea au mti wo wote. Bali wawadhuru wale watu wasiokuwa na muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao. 5 Waliruhusiwa kuwatesa kwa muda wa miezi mitano lakini wasiwaue. Na uchungu wa kuuma kwao ulikuwa kama uchungu wa mtu anapoumwa na nge. 6 Katika siku hizo watu watata futa kifo lakini hawatakiona; watatamani kufa, lakini kifo kita wakimbia.
7 Wale nzige walionekana kama farasi waliotayarishwa kwa vita; vichwani mwao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu; na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu. 8 Manyoya yao yalifanana kama nywele za wanawake; na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. 9 Walikuwa na magamba yaliyofanana na ngao za chuma; na kelele za mabawa yao zilikuwa kama kelele za magari ya farasi yenye farasi wanaokimbia kwenda vitani. 10 Walikuwa na mikia ya kuuma kama nge; nguvu yao ya kutesa watu kwa muda wa miezi mitano ilikuwa katika mikia yao. 11 Walikuwa na mfalme wa kuwatawala, naye ni malaika wa shimo la kuzimu ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Aba doni na kwa Kigiriki ni Apolioni.
12 Maafa ya kwanza yamepita; bado mengine mawili yanakuja.
Tarumbeta Ya Sita
13 Malaika wa sita akapiga tarumbeta yake, nami nikasikia sauti ikitoka katika zile pembe nne za madhabahu iliyoko mbele ya Mungu. 14 Sauti hiyo ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tar umbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa wa Efrati.” 15 Basi wakafunguliwa wale malaika wanne waliokuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo, na siku hiyo na mwezi huo na mwaka huo, wawaue theluthi moja ya wanadamu. 16 Idadi ya majeshi wapandao farasi ilikuwa milioni mia mbili. 17 Na hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: wapanda farasi walivaa ngao vifuani zenye rangi ya moto na samawati na kiberiti. Na vichwa vya farasi hao vilikuwa kama vichwa vya simba; na moto, moshi na kiberiti vili kuwa vinatoka vinywani mwao. 18 Theluthi moja ya wanadamu waliu awa kwa maafa hayo matatu, yaani, moto, moshi na kiberiti, yaliy otoka vinywani mwa hao farasi. 19 Nguvu ya hao farasi ilikuwa vinywani mwao na mikiani mwao; kwa sababu mikia yao ilikuwa kama nyoka wenye vichwa ambavyo vilitumika kuwadhuru watu.
20 Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika maafa hayo, bado walikataa kutubu na kuacha kuabudu vitu walivyotengeneza kwa mikono yao wenyewe. Waliendelea kuabudu pepo, sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, sanamu zisizoweza kuona, kusikia wala kutembea. 21 Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati na wizi.
Copyright © 1989 by Biblica