Ufunua wa Yohana 3-6
Neno: Bibilia Takatifu
Ujumbe Kwa Kanisa La Sardi
3 “Kwa malaika wa Kanisa la Sardi andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako; na kwamba una sifa ya kuwa hai, na kumbe umekufa. 2 Amka! Imarisha kilichobakia kabla hakijaharibika kabisa, kwa maana nimeona kwamba kazi zako hazijakamilika mbele za Mungu wangu. 3 Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na kutubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwizi wala huta jua saa nitakayokujia.
4 Bado wako watu wachache huko Sardi ambao hawajachafua mavazi yao. Wao watatembea pamoja nami wakiwa wamevaa mavazi yao meupe kwa maana wanastahili. 5 Atakayeshinda atavikwa vazi jeupe kama wao, nami sitafuta jina lake katika kitabu cha uzima bali nitalikiri jina lake mbele ya Baba yangu na mbele za malaika wake.
6 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anayaam bia makanisa.”’
Ujumbe Kwa Kanisa La Filadelfia
7 “Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, ambaye anao ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, na anachoki funga hakuna awezaye kukifungua.
8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango ulio wazi ambao hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba ingawa nguvu yako ni ndogo lakini umelishika neno langu na hujalikana jina langu. 9 Sikiliza, wale watu ambao ni wa sinagogi la she tani, wale wajiitao Wayahudi kumbe sio, bali ni waongo; nitawafa nya waje wapige magoti mbele yako na wakiri kwamba nimekupenda. 10 Kwa kuwa umeshika agizo langu la kustahimili kwa subira, nitakulinda wakati wa ile dhiki itakayokuja duniani pote kuwajar ibu waishio ulimwenguni.
11 Ninakuja upesi. Shika sana kile ulicho nacho asije mtu akachukua taji yako. 12 Atakayeshinda nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo kamwe. Na nitaan dika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wake Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unakuja kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Pia nitaandika juu yake jina langu jipya.
13 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anay aambia makanisa.’ ”
Ujumbe Kwa Kanisa La Laodikia
14 “Kwa malaika wa kanisa la Laodikia andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aitwaye Amina, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa vyote alivyoumba Mungu.
15 Nayajua matendo yako; kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali kama ungalikuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa kuwa wewe ni vuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu. 17 Unajigamba ukisema, ‘Mimi ni tajiri , nimefanikiwa wala sihitaji kitu cho chote.’ Lakini hutambui kwamba wewe ni mnyonge, mtu wa kuhurumiwa, maskini, kipofu; tena wewe ni uchi. 18 Kwa hiyo ninakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosaf ishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri; na mavazi meupe ili upate kuvaa, ufiche aibu ya uchi wako. Ujinunulie pia mafuta uyapake macho yako ili upate kuona.
19 Wote niwapendao, ninawakaripia na kuwarudi. Kwa hiyo fanya bidii, utubu na kuziacha dhambi zako. 20 Tazama, nasimama mlangoni napiga hodi. Mtu ye yote akisikia sauti yangu na kufun gua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami. 21 Atakayeshinda nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi. 22 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anay aambia makanisa.’ ”
Kiti Cha Enzi Kilichoko Mbinguni
4 Baada ya hayo nilitazama, nikaona mlango ulio wazi mbin guni. Na ile sauti niliyokuwa nimeisikia ikisema nami kama tar umbeta ikasema, “Njoo huku juu nami nitakuonyesha yatakayotokea baada ya haya. ” 2 Ghafla nilikuwa katika Roho, na mbele yangu kilikuwapo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa. 3 Aliyeketi kwenye kiti hicho cha enzi alionekana kama jiwe zuri jekundu na akiki, na upinde wa mvua ulizunguka kile kiti cha enzi, ukione kana kama zumaridi. 4 Kiti hicho kilizungukwa na viti vingine ishirini na vinne vya enzi ambavyo juu yake walikaa wazee ishi rini na wanne waliokuwa wamevalia mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani. 5 Na katika kile kiti cha enzi kulitoka umeme, ngurumo na sauti. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya kile kiti cha enzi, ambazo ni zile roho saba za Mungu. 6 Mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na kitu kinachofanana na bahari ya kioo iking’aa kama jiwe la kioo. Katikati, kuzunguka kile kiti cha enzi, walikuwapo viumbe hai wanne, wenye macho kila mahali, mbele na nyuma.
7 Kiumbe hai wa kwanza alifanana na simba, wa pili alifanana na ng’ombe dume, wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu, wa nne alifanana na tai arukaye. 8 Na hawa viumbe hai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita na macho kila mahali, hata chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kuimba, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”
9 Kila mara viumbe hao wanne walipomtukuza na kumheshimu na kumshukuru yeye aliyeketi kwenye kiti cha enzi na aishie milele na milele, 10 wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele zake yeye aliyeketi kwenye kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Wakaziweka taji zao mbele ya kile kiti cha enzi wakisema, 11 “Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ni wewe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako vitu vyote viliumbwa na vinapata kuwapo.”
Hati Na Mwana-Kondoo
5 Kisha nikaona katika mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwe nye kile kiti cha enzi hati iliyoandikwa ndani na nje, ambayo ilikuwa imefungwa na mihuri saba. 2 Tena nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, “Ni nani anayestahili kufungua hati hii na kuvunja mihuri yake?” 3 Lakini hakupatikana mtu mbinguni, juu ya nchi, wala chini ya nchi aliyeweza kufungua hati hiyo, wala kuitazama. 4 Nililia sana kwa sababu hakupatikana mtu aliyestahili kuifungua hati hiyo wala kuitazama. 5 Kisha, mmoja wapo wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, yule simba wa kabila la Yuda, wa ukoo wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kufun gua hati hiyo na kuvunja mihuri yake saba.” 6 Katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wanne na wale wazee, nikaona Mwana- Kondoo amesimama, akionekana kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba, na macho saba, ambayo ni wale roho saba wa Mungu waliotumwa ulimwenguni kote . 7 Huyo Mwana-Kondoo akaenda, akaichukua ile hati kutoka kwenye mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi. 8 Alipokwisha kuichukua ile hati, wale viumbe wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ubani , ambao ni maombi ya watu wa Mungu. 9 Nao wakaimba wimbo mpya: “Wewe unastahili kuichukua hati na kuifungua mihuri yake. Kwa sababu wewe uliuawa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila na kila lugha; watu wa kila jamaa na kila taifa. 10 Umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, na watata wala ulimwenguni.” 11 Kisha nikatazama, nikasikia sauti za mal aika wengi sana wakizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wanne na wale wazee ishirini na wanne. Idadi ya hao mal aika ilikuwa ni maelfu na maelfu na kumi elfu mara kumi elfu. 12 Nao waliimba kwa sauti kuu, “Mwana -Kondoo aliyeuawa anasta hili kupewa uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima, na utukufu na sifa!” 13 Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, juu ya nchi na chini ya nchi, baharini na vyote vilivy omo baharini wakiimba, “Baraka na heshima na utukufu na uweza ni wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi; na kwa Mwana-Kondoo, hata milele na milele! 14 Na wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi wakaabudu.
Mwana- Kondoo Avunja Mihuri Saba
6 Kisha nikamwona Mwana -Kondoo akifungua mhuri wa kwanza kati ya ile mihuri saba. Nikasikia mmoja wa wale viumbe wanne akisema kwa sauti kama ya ngurumo: “Njoo!” 2 Nikaangalia, na hapo mbele yangu nikaona farasi mweupe na aliyempanda alikuwa na upinde, na alipewa taji akatoka kama mshindi akaendelee kushinda.
3 Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa pili, nikamsikia yule kiumbe hai wa pili akisema, “Njoo!” 4 Akatoka farasi mwingine mwekundu sana na aliyempanda alipewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye alipewa upanga mkubwa.
5 Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa tatu, nilimsikia yule kiumbe hai wa tatu akisema, “Njoo!” Nikaangalia na mbele yangu nikaona farasi mweusi, na aliyempanda alikuwa na mizani mkononi mwake. 6 Nikasikia kitu kama sauti kati ya hao viumbe wanne hai, ikisema, “Kibaba kimoja cha ngano kwa mshahara wa siku moja! na vibaba vitatu vya shayiri kwa mshahara wa siku moja! Lakini usi haribu mafuta wala divai!”
7 Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa nne, nilisikia sauti ya yule kiumbe hai wa nne ikisema, “Njoo!” 8 Nikaangalia na mbele yangu nikamwona farasi mwenye rangi ya kijivu. Aliyempanda huyo farasi aliitwa mauti, naye alikuwa akifuatana na kuzimu. Nao wal ipewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.
9 Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa tano, niliona chini ya madhabahu, roho za watu waliouawa kwa ajili ya neno la Mungu na kwa ushuhuda wao. 10 Wakalia kwa sauti kuu wakisema, “Bwana Mwenyezi, uliye mtakatifu na mwaminifu, utakawia mpaka lini kuwa hukumu na kulipiza kisasi juu ya watu wote waishio duniani kwa ajili ya damu yetu?” 11 Kisha kila mmoja wao akapewa kanzu nyeupe. Wakaambiwa wasubiri kidogo zaidi mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao wanaopaswa kuuawa kama wao walivyouawa, ita kapotimia.
12 Nilitazama Mwana-Kondoo alipokuwa akifungua muhuri wa sita. Pakatokea tetemeko kuu la nchi na jua likawa jeusi kama gunia lililotengenezwa kwa manyoya ya mbuzi. Mwezi wote ukawa mwekundu kama damu. 13 Nyota zikaanguka ardhini kama vile mat unda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapoti kiswa na upepo mkali. 14 Anga ikatoweka kama vile karatasi inav yosokotwa; na kila mlima na kila kisiwa vikaondolewa mahali pake.
15 Ndipo wafalme wa duniani, wakuu wote, majemadari, mata jiri , wenye nguvu; na kila mtu, mtumwa na aliye huru, wakajifi cha mapangoni na kwenye miamba ya milima. 16 Wakaisihi milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche tusionwe na uso wake yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na mtuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku ile kuu ya ghadhabu yao imekuja, na ni nani awezaye kusalimika?”

Copyright © 1989 by Biblica