Matayo 6
Neno: Bibilia Takatifu
Kuwasaidia Maskini
6 “Angalieni msitende mema mbele ya watu ili muonekane na watu. Kwa maana mkifanya hivyo hamtapata thawabu itokayo kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 “Kwa hiyo mnapowasaidia maskini msitangaze kwa tarumbeta kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani ili wasi fiwe na watu. Nawaambia wazi, wao wamekwisha pata tuzo yao. 3 Lakini ninyi mnapotoa sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kulia unafanya nini; 4 ili sadaka yako iwe ni siri. Naye Baba yako wa mbinguni anayeona sirini ata kupa thawabu.”
Mafundisho Kuhusu Sala
5 “Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. 6 Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu.
7 “Mnaposali msirudie maneno yale yale kama wafanyavyo watu wa mataifa wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasi kilizwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. 8 Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua mahitaji yenu hata kabla hamjaomba.” 9 Basi msalipo ombeni hivi: ‘Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe. 10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupatie leo riziki yetu ya kila siku. 12 Na utusamehe makosa yetu kama sisi tulivyokwisha kuwa samehe waliotukosea. 13 Na usitutie majaribuni, bali utuokoe kutokana na yule mwovu,’ [Kwa kuwa Ufalme na nguvu na utukufu ni vyako milele. Amina.] 14 Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi; 15 lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.
Mafundisho Kuhusu Kufunga
16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao. 17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu 18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.” Akiba Ya Mbinguni. 19 “Msijiwekee mali nyingi duniani ambapo wadudu na kutu huharibu na wezi huvunja na kuiba. 20 Lakini jiwekeeni mali mbinguni ambapo wadudu na kutu hawaharibu na wezi hawavunji na kuiba. 21 Kwa sababu pale akiba yako ilipo ndipo moyo wako uta kapokuwa.”
Jicho Ni Taa Ya Mwili
22 “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zuri, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23 Lakini kama jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Kwa hiyo kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hakika utakuwa na giza la kutisha.”
Mungu Na Mali
24 “Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa sababu, ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au atamthami ni mmoja na kumdharau mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na mali.”
Msiwe Na Wasiwasi
25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege? 27 Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?
28 “Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo. 29 Lakini nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi kuvikwa kama mojawapo la maua hayo. 30 Lakini ikiwa Mungu anay avisha hivi maua ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavisha ninyi vizuri zaidi, enyi watu wenye imani haba? 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Mambo haya ndio yanay owahangaisha watu wa mataifa wasiomjua Mungu; na Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji yote hayo. 33 Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa. 34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”
Matayo 7-12
Neno: Bibilia Takatifu
Usihukumu Wengine
7 Usihukumu ili na wewe usihukumiwe. 2 Kwa maana hukumu uta kayotamka juu ya wenzako ndio itakayotumiwa kukuhukumu, na kipimo utakachotoa ndicho utakachopokea. 3 Kwa nini unaangalia kijiti kidogo kilichomo katika jicho la ndugu yako na wala huoni pande la mti lililoko jichoni mwako? 4 Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Hebu nikutoe uchafu jichoni mwako,’ wakati jichoni mwako mna pande kubwa? 5 Mnafiki wewe! Toa kwanza pande lililoko jichoni mwako, ndipo utaweza kuona vema, upate kukitoa kipande kilichoko ndani ya jicho la ndugu yako.
6 “Msiwape mbwa vitu vitakatifu; na msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe wasije wakazikanyaga kanyaga na halafu wawageukie na kuwashambulia.”
Omba, Tafuta, Bisha Hodi
7 “Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. 8 Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.
9 “Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 12 Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo. Hii ndio maana ya sheria ya Musa na Maandiko ya manabii.”
Njia Nyembamba Na Njia Pana
13 “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana mlango mpana na njia rahisi huelekea kwenye maangamizo, na watu wanaopitia huko ni wengi. 14 Lakini mlango mwembamba na njia ngumu huelekea kwenye uzima, na ni wachache tu wanaoiona.”
Manabii Wa Uongo
15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya na mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni. 20 Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.”
Mfuasi Wa Kweli
21 “Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’
Nyumba Iliyojengwa Kwenye Mwamba
24 “Basi, kila anayesikiliza haya maneno yangu na kuyate keleza, atafanana na mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo uka vuma ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuanguka kwa sababu ili jengwa kwenye msingi imara juu ya mwamba. 26 Na kila anayesikia haya maneno yangu asiyafuate, atafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua ikanyesha, yakatokea mafu riko, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.” 28 Na Yesu alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu waliomsikiliza walishangaa sana, 29 kwa sababu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama walimu wao wa sheria.
Yesu Amponya Mwenye Ukoma
8 Alipotoka mlimani, umati mkubwa wa watu walimfuata. 2 Na mtu mmoja mwenye ukoma akaja akapiga magoti mbele yake akasema, “Bwana, kama ukipenda, unaweza kunitakasa.” 3 Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Napenda. Takasika.” Wakati huo huo yule mtu akapona ukoma wake. 4 Na Yesu akamwambia, “Usiseme cho chote kwa mtu ye yote, lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani na utoe sadaka aliyoamuru Musa, iwe uthibitisho kwa watu kwamba umepona.”
Yesu Amponya Mtumishi Wa Askari
5 Yesu alipoingia Kapernaumu, askari mmoja alikuja kumwomba msaada, 6 akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani ame pooza, tena ana maumivu makali.” 7 Yesu akamwambia, “Nitakuja kumponya.” 8 Lakini yule askari akamwambia, “Bwana, mimi sis tahili wewe uingie nyumbani kwangu; lakini sema neno tu, na mtumi shi wangu atapona. 9 Mimi niko chini ya mamlaka, na ninao askari chini yangu. Nikimwambia askari mmoja ‘Nenda 10 Yesu aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, “Nawaambia kweli, hata katika Israeli sijaona imani ya namna hii. 11 Ninawahakikishia kwamba wengi watatoka mashar iki na magharibi nao wataketi mezani pamoja na Ibrahimu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa mbinguni. 12 Lakini wana wa ufalme watatupwa nje gizani, huko watu watalia na kusaga meno.” 13 Yesu akamwambia yule askari, “Nenda nyumbani, na yale uliy oamini yatimie kwako.” Na yule mtumishi akapona tangu wakati ule ule.
Yesu Aponya Wengi
14 Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wake amelala akiwa ana homa. 15 Akamgusa mkono na homa ikam toka, akaamka akaanza kumhudumia. 16 Jioni ile walimletea watu wengi waliopagawa na pepo; naye akawafukuza pepo kwa neno lake, na akawaponya wagonjwa wote. 17 Miujiza hii ilitimiza yale yali yosemwa na nabii Isaya kwamba: “Alichukua udhaifu wetu, na kubeba magonjwa yetu.”
18 Yesu alipoona umati wa watu unazidi kuongezeka aliwaamuru wanafunzi wake wavuke, waende ng’ambo ya pili. 19 Na mwalimu mmoja wa sheria akamjia Yesu akamwambia, “Mwalimu, mimi nitaku fuata po pote utakapokwenda.” 20 Lakini Yesu akamjibu, “Mbweha wana mashimo yao, na ndege wa angani wana viota vyao, lakini mimi Mwana wa Adamu sina mahali pa kulaza kichwa changu.” 21 Mwana funzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.” 22 Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, waache wal iokufa wawazike wafu wao.”
Yesu Atuliza Dhoruba
23 Alipoingia kwenye mashua wanafunzi wake walimfuata. 24 Mara dhoruba kali ikavuma na mawimbi yakakaribia kuzamisha ile mashua; lakini Yesu alikuwa amelala usingizi. 25 Wanafunzi wake wakaenda kumwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunaangamia!”
26 Lakini Yesu akawajibu, “Enyi wenye imani haba, mbona mnaogopa?” Akasimama, akaikemea dhoruba na mawimbi; navyo vikat ulia, pakawa shwari kabisa. 27 Wanafunzi wake wakashangaa. Wakaulizana, “Ni mtu wa namna gani huyu, ambaye hata upepo na bahari vinamtii?”
28 Walipofika ng’ambo ya Genezareti, watuwawili wenye pepo walikutana naye. Watu hawa waliishi makaburini na walikuwa wanat isha, kiasi kwamba hakuna mtu aliyethubutu kupita njia ile. 29 Wakapiga kelele, “Unataka nini kwetu, wewe Mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kutimia?” 30 Mbali kidogo kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha. 31 Wale pepo wakamsihi Yesu, “Ukitufukuza, tafadhali turuhusu twende kwenye lile kundi la nguruwe.” 32 Akawaambia, “Nendeni”. Basi waka toka wakawaingia wale nguruwe; na kundi lote likatimka mbio kuelekea ukingoni mwa bahari, wakaangamia katika maji. 33 Wachungaji wa hao nguruwe wakakimbilia mjini wakaeleza kila kitu, na yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo. 34 Watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Yesu. Wali pomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.
Yesu Amponya Mtu Aliyepooza
9 Yesu akaingia katika mashua akavuka ziwa, akafika katika mji wa kwao. 2 Watu wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye kitanda chake. Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mtu ali yepooza, “Mwanangu, jipe moyo; dhambi zako zimesamehewa.” 3 Baadhi ya walimu wa sheria wakawaza moyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” 4 Lakini Yesu alifahamu mawazo yao. Akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5 Kwani ni lipi lililo rahisi: kusema ‘Dhambi zako zimesamehewa 6 Lakini, nitawathibitishia kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Akamwambia yule aliyepo oza, “Simama, chukua kitanda chako uende nyumbani.” 7 Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani. 8 Watu walipoyaona haya, wakaogopa, wakamtukuza Mungu ambaye alitoa uwezo wa jinsi hii kwa wanadamu.
Yesu Amwita Mathayo
9 Yesu alipoondoka hapo, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi katika ofisi ya kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate”. Mathayo akainuka, akamfuata. 10 Wakati Yesu alipo kuwa ameketi mezani kula chakula katika nyumba fulani, watoza kodi wengi na wenye dhambi walikuja kula pamoja naye na wanafunzi wake. 11 Mafarisayo walipoona mambo haya wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini mwalimu wenu anakula na watoza kodi na wenye dhambi?” 12 Lakini Yesu alipowasikia aliwaambia, “ Watu wenye afya hawahitaji daktari, lakini wagonjwa wanamhitaji. 13 Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya, ‘Napenda huruma na wala sio sadaka za kuteketeza.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”
Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga
14 Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walikuja kwa Yesu wakamwuli za, “Mbona sisi na Mafarisayo tunafunga lakini wanafunzi wako hawafungi?” 15 Yesu akawajibu, “Hivi inawezekana wageni wali oalikwa harusini kuomboleza wakati bwana harusi yuko nao? Wakati utafika ambapo bwana harusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo wataka pofunga. 16 Hakuna mtu anayeweka kiraka kipya kwenye nguo kuu kuu, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye nguo hiyo na tundu litakalotokea litakuwa kubwa zaidi ya lile la mwanzo. 17 Wala watu hawahifadhi divai mpya kwenye viriba vikuukuu; wakifanya hivyo, viriba vitapasuka na divai itamwagika. Lakini divai mpya huwekwa katika viriba vipya na kwa njia hiyo divai na viriba husalimika.”
Yesu Amponya Mwanamke Aliyetokwa Damu
18 Wakati Yesu akiwa anawaambia haya, akaja afisa fulani akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amefariki lakini tafadhali uje umwekee mkono wako juu yake naye atakuwa hai.” 19 Yesu akasimama akamfuata. Wanafunzi wake pia wakaan damana naye.
20 Akatokea mwanamke mmoja ambaye alikuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu akagusa upindo wa nguo yake, 21 kwa maana alisema moyoni mwake, “Nikigusa tu nguo yake, nitaponywa.” 22 Yesu akageuka, na alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo, imani yako imekuponya.” Na wakati huo huo yule mwanamke akapona.
Yesu Amfufua Binti Wa Afisa
23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule afisa, aliwakuta waom bolezaji wanapiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele. 24 Akawaambia, “Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala.” Wakamcheka kwa dhihaka. 25 Lakini watu walipok wisha tolewa nje, aliingia ndani akamshika mkono yule binti, naye akaamka. 26 Habari hizi zikaenea wilaya ile yote.
Yesu Aponya Vipofu
27 Yesu alipoondoka pale, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele kwa nguvu, “Mwana wa Daudi, tuhurumie.” 28 Alipoingia ndani wale vipofu walimfuata. Akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kuwafanya muone?” Wakamjibu, “Ndio Bwana.” 29 Ndipo Yesu akagusa macho yao akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyo amini.” 30 Macho yao yakafunguka. Naye akawaonya, “Angalieni mtu ye yote asijue jambo hili.” 31 Lakini wao walipoondoka walieneza sifa zake katika ile wilaya yote.
Yesu Amponya Bubu
32 Walipokuwa wakiondoka, watu walimletea mtu bubu, ali yekuwa amepagawa na pepo. 33 Na yule pepo alipofukuzwa, yule aliyekuwa bubu aliweza kusema. Ule umati wa watu wakastaajabu, wakasema, “Jambo kama hili halijawahi kuonekana katika Israeli.” 34 Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo kwa uwezo wa mkuu wa pepo.”
Wafanyakazi Ni Wachache
35 Yesu akazunguka kwenye miji yote na vijiji vyote akifundi sha katika masinagogi na kuhubiri Habari Njema za Ufalme, na kuponya kila ugonjwa na kila udhaifu. 36 Alipoona umati wa watu, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanateseka pasipo msaada, kama kondoo wasio na mchungaji.
37 Akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini wafa nyakazi ni wachache; 38 basi mwombeni Bwana wa mavuno ili awape leke wafanyakazi kwenye mavuno yake.”
Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili
10 Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka ya kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. 2 Majina ya hao wanafunzi kumi na wawili ni haya: 3 wa kwanza, Simon, ambaye aliitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo, mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; Filipo na Bartholomayo; Tomaso na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; 4 Simoni Mkanaani; na Yuda Iskariote ambaye baadaye alimsaliti Yesu. 5 Yesu aliwatuma hawa kumi na wawili, akawaagiza, “Msiende kwa watu wa mataifa wala msiingie mji wo wote wa Wasamaria. 6 Bali waendeeni kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. 7 Na mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia; 8 Waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepo kea bure, toeni bure. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha wala sarafu za shaba katika mikanda yenu. 10 Msichukue mikoba ya safari, wala koti la pili, wala viatu, wala fimbo: kwa maana mfanyakazi anastahili riziki yake.
11 “Mkiingia katika mji au kijiji cho chote, mtafuteni mtu mwaminifu mkae kwake mpaka mtakapoondoka. 12 Kila nyumba mtakay oingia, toeni salamu. 13 Kama watu wa nyumba hiyo wanastahili, amani yenu na ikae kwao; na kama hawastahili, amani yenu itawaru dia ninyi. 14 Na kama mtu ye yote akikataa kuwapokea au kusiki liza maneno yenu, mtakapoondoka katika nyumba hiyo au mji huo, kung’uteni mavumbi yatakayokuwa miguuni mwenu. 15 Nawaambieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma na Gomora kuliko itakavyokuwa kwa mji huo.”
Yesu Awatayarisha Wanafunzi Wake Kwa Mateso
16 “Ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua. 17 Jihadharini na watu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga viboko kwenye masinagogi yao. 18 Mtapelekwa mbele ya magavana na wafalme kwa ajili yangu mkatoe ushuhuda mbele yao na mbele ya watu wa mataifa. 19 Lakini mtakapokamatwa, msihangaike mkifiki ria mtakalosema; kwa maana mtaambiwa la kusema wakati huo. 20 Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkizungumza bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akisema kupitia kwenu. 21 Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanae auawe. Watoto nao wataasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 22 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ataokoka. 23 Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kwa maana nawaambieni hakika, hamtamaliza kuipitia miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu hajafika.
24 “Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake wala mtumishi hamzidi bwana wake. 25 Inatosha ikiwa mwanafunzi atakuwa kama mwalimu wake na mtumishi kama bwana wake. Ikiwa wamethubutu kum wita bwana mwenye nyumba Beelzebuli, je, si watawasema vibaya zaidi jamaa ya mwenye nyumba?”
Anayestahili Kuogopwa
27 Ninalo waambia gizani, ninyi litamkeni mwangani: na lile mnalosikia likinong’onwa, litangazeni mkiwa mmesimama kwenye paa la nyumba. 28 Msiwaogope wale wawezao kuua mwili lakini hawawezi kuua roho; ila mwogopeni yeye ambaye anaweza kuiangamiza roho na mwili katika moto wa Jehena. 29 Mbayuwayu wawili huuzwa kwa sarafu moja tu. Lakini hata mmoja wao hawezi kuanguka pasipo Baba yenu kupenda. 30 Hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa. 31 Kwa hiyo msiogope; kwa maana ninyi mna thamani kubwa zaidi kuliko mbayuwayu wengi. 32 Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 33 Lakini ye yote atakayenikana mbele ya watu, mimi pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.”
Gharama Ya Kumfuata Yesu
34 “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali vita. 35 Kwa maana nimekuja kuleta kutokuele wana kati ya mtu na baba yake, na kati ya binti na mama yake, na kati ya mkwe na mama mkwe wake. 36 Na maadui wakubwa wa mtu watakuwa watu wa nyumbani kwake. 37 Ye yote anayempenda baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Na ye yote ampendaye mwanae au binti yake kuliko anavyoni penda mimi, hastahili kuwa wangu. 38 Na ye yote asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. 39 Ata kayeng’ang’ania nafsi yake ataipoteza lakini aipotezae nafsi yake kwa ajili yangu ataipata.”
Watakaopokea Tuzo
40 “Mtu ye yote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi; na ye yote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye ali yenituma. 41 Mtu anayemkaribisha nabii kwa kuwa ni nabii, atapo kea tuzo ya nabii; na mtu anayemkaribisha mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapokea tuzo ya mwenye haki. 42 Na mtu ata kayetoa japo kikombe cha maji kwa mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, basi ninawaambieni hakika, hatakosa tuzo yake.”
Yohana Atuma Wanafunzi Wake Kwa Yesu
11 Yesu alipomaliza kutoa maagizo yake kwa wale wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka pale akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. 2 Basi Yohana Mbatizaji aliposikia akiwa gere zani mambo ambayo Yesu alikuwa akifanya, aliwatuma wanafunzi wake 3 wakamwulize, “Wewe ni yule anayekuja, au tumngojee mwin gine?” 4 Yesu akawajibu, “Nendeni mkamweleze Yohana yale mnayo sikia na kuona: 5 vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema. 6 Amebarikiwa mtu ambaye hapotezi imani yake kwangu.”
7 Wale wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuwaam bia ule umati wa watu kuhusu Yohana Mbatizaji. Akawauliza, “Mli pokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? 8 Kama sivyo, mlikwenda huko kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi maridadi? Lakini wanaovaa nguo maridadi wanakaa katika majumba ya wafalme. 9 Basi kwa nini mlikwenda huko? Kumwona nabii? Naam, nawaambieni yeye ni zaidi ya nabii. 10 Huyo ndiye ambaye anaelezwa katika Maandiko kwamba: ‘ Angalia namtuma mjumbe mbele yako, ambaye atakuandalia njia.’ 11 Nawaambieni kweli kwamba kati ya watu wote waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu zaidi ya Yohana Mbatizaji. Lakini hata hivyo aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni, ni mkuu kuliko Yohana. 12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mungu umekuwa ukishambuliwa vikali; na watu wenye jeuri wanajaribu kuuteka kwa nguvu. 13 Kwa maana manabii wote na sheria walita biri mpaka wakati wa Yohana. 14 Na kama mko tayari kusadiki uta biri wao, basi Yohana ndiye Eliya ambaye kuja kwake kulitabiriwa. 15 Mwenye nia ya kusikia na asikie.
16 “Kizazi hiki nikilinganishe na nini?” Kinafanana na waliokaa masokoni wakiwaita wenzao na kuwaambia, 17 ‘Tuliwapigia filimbi, lakini hamkucheza; tuliwaimbia nyimbo za msiba, lakini hamkuomboleza.’ 18 Kwa maana Yohana Mbatizaji alikuja na akawa hali wala hanywi nao wanasema, ‘Amepagawa na pepo’. 19 Mimi mwana wa Adamu nimekuja nikila na kunywa, nao wanasema, ‘Mta zameni mlafi na mlevi; rafiki wa watoza kodi na wenye dhambi!’ Lakini hekima huthibitishwa kwa matendo yake.”
Ole Kwa Korazini Na Bethsaida
20 Yesu akaanza kuikemea miji ambamo alifanya matendo mengi ya ajabu kwa maana watu wake hawakutubu. 21 “Ole wenu watu wa Korazini! Ole wenu watu wa Bethsaida! Kwa maana kama matendo makuu yaliyofanyika kwenye miji yenu yangelifanyika Tiro na Sidoni, watu wa huko wangelikuwa wametubu tangu zamani na kuvaa magunia na kujipaka majivu, kudhihirisha kujuta kwao. 22 Lakini nawaambia, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Tiro na Sidoni kuliko itakavyokuwa kwenu. 23 Na ninyi watu wa Kapernaumu, mnadhani mtainuliwa hadi juu mbinguni? Mtashushwa hadi kuzimuni. Kwa kuwa kama mambo makuu yaliyofanyika kwenu yangalifanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwapo hadi leo. 24 Lakini nawaam bieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma kuliko itakavyokuwa kwenu.”
Hakuna Amjuaye Baba Ila Mwana
25 Wakati huo Yesu alisema, “Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, na ukawafunulia watoto wachanga. 26 Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. 27 Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: na hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na mtu ye yote ambaye Mwana anapenda kumdhihirisha Baba kwake.”
Yesu Awaita Waliolemewa Na Mizigo
28 “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu; jifunzeni kutoka kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni rahisi, na mzigo wangu ni mwepesi.”
Yesu Ni Bwana Wa Sabato
12 Wakati huo Yesu alipitia kwenye mashamba ya ngano siku ya sabato. Wanafunzi wake walikuwa na njaa, wakaanza kuvunja masuke ya ngano na kula. 2 Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili wakam wambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanya siku ya sabato.”
3 Yesu akawajibu, “Hamjasoma walichofanya Daudi na wafuasi wake walipokuwa na njaa? 4 Waliingia katika nyumba ya Mungu wakala mkate uliowekwa wakfu, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya isipokuwa makuhani peke yao. 5 Au hamjasoma katika sheria kwamba siku ya sabato makuhani huvunja sheria ya sabato Hekaluni lakini hawahesabiwi kuwa na hatia? 6 Nawaambieni wazi kwamba, aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa. 7 Na kama mngalifahamu maana ya maneno haya, ‘Ninataka rehema wala si sadaka ya kuteketezwa;’ msingeliwalaumu watu wasio na hatia, 8 kwa maana Mwana wa Adamu ni Bwana wa sabato.”
Yesu Anamponya Mtu Aliyepooza Mkono
9 Yesu alipoondoka hapo, aliingia katika sinagogi lao. Huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono . 10 Wakitafuta sababu ya kumsh taki, wakamwuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya sabato?” 11 Yesu akawajibu, “Ni nani kati yenu ambaye kondoo wake aki tumbukia shimoni siku ya sabato hatamtoa? 12 Mtu ana thamani kubwa sana kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya sabato.”
13 Ndipo akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akau nyoosha, nao ukapona ukawa mzima kama ule mwingine. 14 Lakini Mafarisayo wakatoka nje wakashauriana jinsi ya kumwangamiza
Mtumishi Aliyechaguliwa Na Mungu
15 Lakini Yesu akiyafahamu mawazo yao, aliondoka mahali hapo. Na watu wengi walimfuata naye akawaponya wote. 16 Akawa kataza wasimtangaze. 17 Hii ilikuwa ili yatimie maneno aliyosema nabii Isaya: 18 “Mtazameni mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu ambaye moyo wangu unapendezwa naye. Nitaweka Roho yangu juu yake , naye atatangaza haki kwa watu wa mataifa. 19 Hatabishana wala hatapiga kelele, sauti yake haitasikika mitaani. 20 Hataponda unyasi uliochubuliwa wala hatazima mshumaa unaokaribia kuzima, mpaka atakapoifanya haki ipate ushindi; 21 na watu wa mataifa wataweka tumaini lao katika jina lake.”
Yesu Na Beelzebuli
22 Kisha wakamletea kipofu mmoja ambaye pia alikuwa bubu na amepagawa na pepo. Yesu akamponya akaweza kusema na kuona. 23 Watu wote wakashangaa wakaulizana, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?” 24 Lakini Mafarisayo waliposikia haya wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mfalme wa pepo wote.”
25 Yesu alifahamu mawazo yao, akawaambia, “Utawala wo wote ambao umegawanyika wenyewe kwa wenyewe utaanguka. Hali kadhalika mji wo wote au jamaa ye yote iliyogawanyika yenyewe kwa yenyewe haitadumu. 26 Na kama shetani anamfukuza shetani, atakuwa amega wanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utaendeleaje? 27 Na kama mimi hutoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, watu wenu je, wao hutoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao ndio watakaowaamulia. 28 Lakini kama ninatoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia. 29 Au inawezekanaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang’anya mali yake yote pasipo kwanza kumfunga yule mwenye nguvu? Akisha mfunga ndipo hakika anaweza kupora mali yake.
30 “Mtu asiyekuwa pamoja nami ananipinga; na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, anatawanya. 31 Kwa hiyo nawaambieni, watu watasamehewa kila aina ya dhambi na kufuru lakini mtu ata kayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.
32 “Na mtu atakayesema neno kumpinga Mwana wa Adamu ata samehewa, lakini ye yote atakayempinga Roho Mtakatifu hatasame hewa, katika ulimwengu huu wala katika ulimwengu ujao.”
Maneno Huonyesha Hali Ya Moyo
33 “Ili upate matunda mazuri lazima uwe na mti mzuri; ukiwa na mti mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulikana kwa matunda yake. 34 Ninyi uzao wa nyoka! Mnawe zaje kunena mema wakati ninyi ni waovu? Kwa maana mtu husema yaliyojaa moyoni mwake. 35 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutokana na hazina ya wema uliohifadhiwa ndani yake; na mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutokana na hazina ya uovu uliohifadhiwa ndani yake.
36 “Nawaambia hakika, siku ya hukumu watu watatakiwa kujieleza kuhusu kila neno lisilo la maana walilolisema. 37 Kwa maana kutokana na maneno yako utahesabiwa haki, na kutokana na maneno yako utahukumiwa.”
Ishara Ya Yona
38 Kisha baadhi ya waandishi wa sheria na Mafarisayo wakam wambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” 39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi cha watu waovu na wasiowaami nifu hutafuta ishara; lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi. 41 Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu wakati Yona alipowahubiria, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki; kwa kuwa yeye alisafiri kutoka miisho ya dunia ili akaisikilize hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.”
Mafundisho Kuhusu Pepo Mchafu
43 “Pepo mchafu akimtoka mtu, huzunguka sehemu kame akita futa mahali pa kupumzika, lakini hapati. 44 Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye ile nyumba yangu nilikotoka.’ Na anaporudi, anaikuta ile nyumba ikiwa tupu, imefagiliwa na kupangwa vizuri.
Copyright © 1989 by Biblica