Add parallel Print Page Options

Yesu Amweka Huru Mvulana Kutoka Pepo Mchafu

(Mk 9:14-29; Lk 9:37-43a)

14 Yesu na wafuasi walirudi kwa watu. Mtu mmoja akamjia Yesu na kuinama mbele zake. 15 Akasema, “Bwana, umwonee huruma mwanangu. Anateswa sana na kifafa alichonacho. Anaangukia kwenye moto au maji mara kwa mara. 16 Nilimleta kwa wafuasi wako, lakini wameshindwa kumponya.”

17 Yesu akajibu, “Ninyi watu mnaoishi katika nyakati hizi cha kizazi kisicho na imani. Maisha yenu ni mabaya sana! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kijana hapa.” 18 Yesu akamwamuru pepo aliye ndani ya kijana, na pepo akamtoka na yule kijana akapona.

Read full chapter

Yesu Amponya Kijana Mwenye Kifafa

14 Alipofikia ulipokuwa umati wa watu, mtu mmoja alimjia Yesu akapiga magoti mbele yake akasema, 15 “Bwana, mwonee huruma mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara nyingi huan guka motoni na kwenye maji. 16 Nimemleta kwa wanafunzi wako laki ni hawakuweza kumponya.”

17 Yesu akajibu, “Ninyi kizazi kipotovu msioamini, nitakaa nanyi mpaka lini na nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kijana hapa kwangu.” 18 Yesu akamkemea yule pepo mchafu, akamtoka yule kijana, naye akapona tangu wakati huo.

Read full chapter