Add parallel Print Page Options

12 Furahini na kushangilia kwa sababu thawabu kuu inawasubiri mbinguni. Furahini kwa kuwa ninyi ni kama manabii walioishi zamani. Watu waliwatendea wao mambo mabaya kama haya pia.

Ninyi ni Kama Chumvi na Nuru

(Mk 9:50; 4:21; Lk 14:34-35; 8:16)

13 Mnahitajika kama chumvi inavyohitajiwa na wale waliopo duniani. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezi kufanywa chumvi tena. Haina manufaa yo yote isipokuwa hutupwa nje na kukanyagwa na watu.

14 Ninyi ni nuru inayong'aa ili ulimwengu uweze kuiona. Ni kama mji uliojengwa juu ya kilima unavyoonekana wazi.

Read full chapter