Mathayo 5:11-13
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
11 Heri kwenu ninyi pale watu watakapowatukana na kuwatesa. Watakapodanganya na akasema kila neno baya juu yenu kwa kuwa mnanifuata mimi. 12 Furahini na kushangilia kwa sababu thawabu kuu inawasubiri mbinguni. Furahini kwa kuwa ninyi ni kama manabii walioishi zamani. Watu waliwatendea wao mambo mabaya kama haya pia.
Ninyi ni Kama Chumvi na Nuru
(Mk 9:50; 4:21; Lk 14:34-35; 8:16)
13 Mnahitajika kama chumvi inavyohitajiwa na wale waliopo duniani. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezi kufanywa chumvi tena. Haina manufaa yo yote isipokuwa hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Read full chapter
Matayo 5:11-13
Neno: Bibilia Takatifu
11 Mmebarikiwa ninyi wakati watu watakapowatukana na kuwatesa na kuwasingizia maovu kwa ajili yangu. 12 Shangilieni na kufurahi, kwa maana zawadi yenu huko mbinguni ni kubwa; kwa kuwa ndivyo walivyowatesa manabii waliowatangulia ninyi.
13 “Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezekani kuwa chumvi tena. Haifai kwa kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.
Read full chapter© 2017 Bible League International
Copyright © 1989 by Biblica