Font Size
Matendo Ya Mitume 24:23-25
Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 24:23-25
Neno: Bibilia Takatifu
23 Akaamuru askari amweke Paulo kizuizini chini ya ulinzi lakini awe na uhuru kiasi, na marafiki zake wasizuiwe kumhudumia. 24 Baada ya siku chache Feliksi akaja na mkewe Drusila ambaye alikuwa Myahudi. Akatuma Paulo aitwe, wakamsikiliza akizungumza juu ya kumwamini Kristo Yesu. 25 Na Paulo alipokuwa akiwaeleza juu ya kuwa na kiasi na juu ya hukumu ya mwisho, Feliksi aliin giwa na hofu akasema, “Tafadhali sasa nenda, nitakuita tena nikipata nafasi.”
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica