Matendo Ya Mitume 13
Neno: Bibilia Takatifu
Barnaba Na Sauli Wachaguliwa Kwa Kazi Maalumu
13 Katika Kanisa la Antiokia Walikuwako manabii na waalimu wafuatao: Barnaba, Simeoni aitwaye mtu mweusi, Lukio kutoka Kirene, Manaeni aliyekuwa nduguye mfalme Herode, na Sauli. 2 Wal ipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu aliwaambia, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi maalumu niliyowaitia.” 3 Kwa hiyo baada ya kufunga na kuomba, waliwawekea mikono Sauli na Barnaba wakawaaga.
Barnaba Na Sauli Waenda Kipro
4 Barnaba na Sauli wakaongozwa na Roho Mtakatifu wakaenda mpaka Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro . 5 Nao walipowasili katika mji wa Salami, walihubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Walikuwa wameongozana na Yohana Marko kama msaidizi wao.
Bar-Yesu Alaaniwa Na Mitume
6 Baada ya kuhubiri sehemu zote za kisiwa cha Kipro walifika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, aitwaye Bar-Yesu. 7 Bar-Yesu alikuwa rafiki wa liwali ait waye Sergio Paulo, mtu mwenye hekima. Liwali huyu alituma Sauli na Barnaba waletwe kwake kwa sababu alitaka kusikia Neno la Mungu. 8 Lakini yule mchawi ambaye jina lake kwa Kigiriki ni Elima, alijaribu kuwapinga Barnaba na Sauli na kumshawishi yule liwali asiwasikilize. 9 Ndipo Sauli ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho yule mchawi, 10 akamwambia, “Wewe mwana wa Shetani! Wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa hila, na uovu. Je, utaacha lini kujaribu kugeuza kweli ya Bwana kuwa uongo? 11 Na sasa tazama mkono wa Bwana uko juu yako kukuadhibu, nawe utakuwa kipofu; hutaona kwa muda.” Na mara ukungu na giza likafunika macho ya Elima akaanza kutanga-tanga akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwonyeshe njia. 12 Yule liwali alipoona mambo haya, akaamini, kwa maana alistaajabishwa na mafundisho ya Bwana.
13 Basi Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo mpaka Perge huko Pamfilia. Yohana Marko akawaacha huko akarejea Yerusalemu. 14 Lakini Barnaba na Paulo wakaendelea hadi Antiokia, mji ulioko katika jimbo la Pisidia. Na siku ya sabato waliingia ndani ya sinagogi wakaketi . 15 Baada ya kusoma kutoka katika vitabu vya sheria za Musa na Maandiko ya manabii, viongozi wa lile sinagogi waliwatumia ujumbe pale walipokaa wakisema, “Ndugu, kama mna neno la mafundisho kwetu, njooni mkaliseme watu walisikie. 16 Paulo akasimama akawapungia mkono akasema, “Watu wa Israeli, na ninyi wote mnaomcha Mungu, sikilizeni. 17 Mungu wa taifa la Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kuwa taifa kubwa wakati walipoishi katika nchi ya Misri na akawatoa katika utumwa wa Misri kwa nguvu za ajabu. 18 Kwa muda wa miaka arobaini aliwavu milia walipokuwa jangwani. 19 Na baada ya kuwaangamiza mataifa saba waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao kwa muda wa miaka mia nne na hamsini. 20 Kisha akawapa Waamuzi wakatawala mpaka wakati wa nabii Samweli. 21 Hatimaye wakataka wawe na mfalme. Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, wa kabila la Benjamini, akawatawala kwa miaka arobaini. 22 Mungu akamwondoa Sauli katika ufalme, akamta waza Daudi mwana wa Yese, akamshuhudia akisema, ‘Nimempata Daudi mwana wa Yese, ambaye moyo wangu unapendezwa naye. Yeye atafanya mapenzi yangu .’ 23 Katika uzao wa Daudi, Mungu amewaletea Wais raeli mkombozi, Yesu, kama alivyoahidi. 24 Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri ubatizo wa toba kwa watu wote wa Israeli. 25 Kabla Yohana Mbatizaji hajamaliza kazi yake, alisema, ‘Mna nidhania mimi ni nani? Mimi siye yule mnayemtazamia. Lakini anayekuja baada yangu mimi sistahili hata kufungua viatu vyake.’
26 “Ndugu zangu, wana wa Ibrahimu, na ninyi mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu ni kwa ajili yetu. 27 Watu wa Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua Yesu kuwa ni Mwokozi. Lakini kwa kum hukumu kifo walitimiza maneno ya manabii yaliyokuwa yaliyokuwa yakisomwa kila siku ya sabato. Hata hivyo wameyafanya maneno ya manabii kutimilika walipomshitaki Yesu. 28 Ijapo kuwa hawakupata sababu yo yote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato amtoe auawe. 29 Na baada ya kufanya kila kitu kilichotabiriwa katika Maandiko kumhusu, wakamshusha kutoka msalabani wakamweka kaburini. 30 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. 31 Na kwa siku nyingi akawatokea wale waliosafiri naye kutoka Galilaya kwenda Yerusalemu. Wao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wote.
32 “Nasi tunawaletea Habari Njema kwamba yale Mungu aliy oahidi baba zetu, 33 sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya Pili, ‘Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa baba yako.’ 34 Na kuhusu kufufuka kwake, na kwamba hataona tena uharibifu, Mungu alisema hivi, ‘Nitakupa wewe baraka takatifu za hakika ambazo nilimwahidi Daudi.’ 35 Na pia Maandiko yanasema katika sehemu nyingine, ‘Wewe hutaruhusu Mtakatifu wako aone uharibifu.’ 36 Kwa maana Daudi alipokwisha kamilisha mapenzi ya Mungu katika kizazi chake, alikufa akazikwa pamoja na baba zake, mwili wake ukaharibika. 37 Lakini yule ambaye Mungu alimwinua kutoka kwa wafu, mwili wake haukuharibika. 38 Kwa hiyo ndugu zangu, fahamuni kwamba katika huyu Yesu, msa mahawa dhambi unatangazwa kwenu. 39 Kwa ajili yake, kila mtu amwaminiye anawekwa huru na yale yote ambayo sheria ya Musa haikuweza kuwaweka huru. 40 Kwa hiyo jihadharini ili yale waliy osema manabii yasiwapate: 41 ‘Tazameni ninyi wenye kudharau, mkapate kushangaa na kuangamia kwa maana nitatenda jambo wakati wenu, ambalo hamtalisadiki, hata kama mtu akiwatangazia.’
42 Barnaba na Paulo walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi watu waliwasihi warudi tena sabato ifuatayo wawaambie zaidi kuhusu mambo haya. 43 Baada ya mkutano wa sinagogi kumalizika Wayahudi wengi na waongofu wa dini ya Kiyahudi waliwafuata Paulo na Bar naba, nao wakazungumza na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu. 44 Sabato iliyofuata karibu watu wote wa mji ule walikuja kusikiliza neno la Mungu. 45 Lakini Wayahudi walipoona lile kusanyiko kubwa la watu, waliona wivu, wakakanusha mafundisho ya Paulo na kumtukana. 46 Paulo na Barnaba wakazidi kufundisha kwa ujasiri, wakisema, “Ilikuwa ni lazima neno la Mungu lihubiriwe kwanza kwenu Wayahudi. Lakini kwa kuwa mnalikataa, mnajihukumu wenyewe kuwa hamstahili kupata uzima wa milele. Tutawahubiria watu wa mataifa mengine. 47 Kwa maana Bwana ametuagiza akisema, ‘Nimewaweka ninyi kuwa nuru kwa watu wa mataifa, ili mpeleke wokovu hadi pembe zote za dunia.”’ 48 Watu wa mataifa mengine waliposikia maneno haya walifurahi, wakalitukuza neno la Mungu; na wote waliochaguliwa kwa ajili ya uzima wa milele wakaamini. 49 Neno la Mungu likaenea sehemu zote katika jimbo lile. 50 Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake waheshimiwa wamchao Mungu pamoja na viongozi maarufu wa mji, wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba na kisha wakawafukuza kutoka wilaya ile. 51 Paulo na Barnaba wakakung’uta mavumbi miguuni mwao kuwapinga, wakaenda mji wa Ikonio. 52 Na Wanafunzi wakajazwa na furaha ya Roho Mtaka tifu.
Copyright © 1989 by Biblica