Matayo 19:16-26
Neno: Bibilia Takatifu
Mtu Tajiri
16 Mtu mmoja alikuja kwa Yesu akamwuliza, “Mwalimu, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?”
17 Yesu akamjibu, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema . Lakini kama unataka kuingia uzimani, tii amri.”
18 Yule mtu akamwuliza, “Amri zipi?” Yesu akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, 19 waheshimu baba yako na mama yako na umpende jirani yako kama nafsi yako.”
20 Yule kijana akasema, “Zote hizi nimezitii. Ninapungukiwa na nini zaidi?”
21 Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda kauze vitu vyote ulivyo navyo na fedha utakazopata uwape maskini, nawe utakuwa umejiwekea hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.” 22 Yule kijana aliposikia hayo aliondoka kwa masikitiko, kwa sababu alikuwa tajiri sana.
Hatari Za Utajiri
23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, “Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni. 24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.” 25 Wanafunzi wake waliposikia haya walishangaa sana, wakamwuliza, “Ni nani basi anaweza kuokoka?” 26 Lakini Yesu akawatazama akawaambia, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.”
Read full chapter

Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica