Yohana Atuma Wanafunzi Wake Kwa Yesu

11 Yesu alipomaliza kutoa maagizo yake kwa wale wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka pale akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. Basi Yohana Mbatizaji aliposikia akiwa gere zani mambo ambayo Yesu alikuwa akifanya, aliwatuma wanafunzi wake wakamwulize, “Wewe ni yule anayekuja, au tumngojee mwin gine?” Yesu akawajibu, “Nendeni mkamweleze Yohana yale mnayo sikia na kuona: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema. Amebarikiwa mtu ambaye hapotezi imani yake kwangu.”

Wale wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuwaam bia ule umati wa watu kuhusu Yohana Mbatizaji. Akawauliza, “Mli pokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? Kama sivyo, mlikwenda huko kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi maridadi? Lakini wanaovaa nguo maridadi wanakaa katika majumba ya wafalme. Basi kwa nini mlikwenda huko? Kumwona nabii? Naam, nawaambieni yeye ni zaidi ya nabii. 10 Huyo ndiye ambaye anaelezwa katika Maandiko kwamba: ‘ Angalia namtuma mjumbe mbele yako, ambaye atakuandalia njia.’ 11 Nawaambieni kweli kwamba kati ya watu wote waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu zaidi ya Yohana Mbatizaji. Lakini hata hivyo aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni, ni mkuu kuliko Yohana. 12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mungu umekuwa ukishambuliwa vikali; na watu wenye jeuri wanajaribu kuuteka kwa nguvu. 13 Kwa maana manabii wote na sheria walita biri mpaka wakati wa Yohana. 14 Na kama mko tayari kusadiki uta biri wao, basi Yohana ndiye Eliya ambaye kuja kwake kulitabiriwa. 15 Mwenye nia ya kusikia na asikie.

16 “Kizazi hiki nikilinganishe na nini?” Kinafanana na waliokaa masokoni wakiwaita wenzao na kuwaambia, 17 ‘Tuliwapigia filimbi, lakini hamkucheza; tuliwaimbia nyimbo za msiba, lakini hamkuomboleza.’ 18 Kwa maana Yohana Mbatizaji alikuja na akawa hali wala hanywi nao wanasema, ‘Amepagawa na pepo’. 19 Mimi mwana wa Adamu nimekuja nikila na kunywa, nao wanasema, ‘Mta zameni mlafi na mlevi; rafiki wa watoza kodi na wenye dhambi!’ Lakini hekima huthibitishwa kwa matendo yake.”

Ole Kwa Korazini Na Bethsaida

20 Yesu akaanza kuikemea miji ambamo alifanya matendo mengi ya ajabu kwa maana watu wake hawakutubu. 21 “Ole wenu watu wa Korazini! Ole wenu watu wa Bethsaida! Kwa maana kama matendo makuu yaliyofanyika kwenye miji yenu yangelifanyika Tiro na Sidoni, watu wa huko wangelikuwa wametubu tangu zamani na kuvaa magunia na kujipaka majivu, kudhihirisha kujuta kwao. 22 Lakini nawaambia, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Tiro na Sidoni kuliko itakavyokuwa kwenu. 23 Na ninyi watu wa Kapernaumu, mnadhani mtainuliwa hadi juu mbinguni? Mtashushwa hadi kuzimuni. Kwa kuwa kama mambo makuu yaliyofanyika kwenu yangalifanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwapo hadi leo. 24 Lakini nawaam bieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma kuliko itakavyokuwa kwenu.”

Hakuna Amjuaye Baba Ila Mwana

25 Wakati huo Yesu alisema, “Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, na ukawafunulia watoto wachanga. 26 Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. 27 Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: na hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na mtu ye yote ambaye Mwana anapenda kumdhihirisha Baba kwake.”

Yesu Awaita Waliolemewa Na Mizigo

28 “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu; jifunzeni kutoka kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni rahisi, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Yesu Ni Bwana Wa Sabato

12 Wakati huo Yesu alipitia kwenye mashamba ya ngano siku ya sabato. Wanafunzi wake walikuwa na njaa, wakaanza kuvunja masuke ya ngano na kula. Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili wakam wambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanya siku ya sabato.”

Yesu akawajibu, “Hamjasoma walichofanya Daudi na wafuasi wake walipokuwa na njaa? Waliingia katika nyumba ya Mungu wakala mkate uliowekwa wakfu, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya isipokuwa makuhani peke yao. Au hamjasoma katika sheria kwamba siku ya sabato makuhani huvunja sheria ya sabato Hekaluni lakini hawahesabiwi kuwa na hatia? Nawaambieni wazi kwamba, aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa. Na kama mngalifahamu maana ya maneno haya, ‘Ninataka rehema wala si sadaka ya kuteketezwa;’ msingeliwalaumu watu wasio na hatia, kwa maana Mwana wa Adamu ni Bwana wa sabato.”

Yesu Anamponya Mtu Aliyepooza Mkono

Yesu alipoondoka hapo, aliingia katika sinagogi lao. Huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono . 10 Wakitafuta sababu ya kumsh taki, wakamwuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya sabato?” 11 Yesu akawajibu, “Ni nani kati yenu ambaye kondoo wake aki tumbukia shimoni siku ya sabato hatamtoa? 12 Mtu ana thamani kubwa sana kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya sabato.”

13 Ndipo akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akau nyoosha, nao ukapona ukawa mzima kama ule mwingine. 14 Lakini Mafarisayo wakatoka nje wakashauriana jinsi ya kumwangamiza

Mtumishi Aliyechaguliwa Na Mungu

15 Lakini Yesu akiyafahamu mawazo yao, aliondoka mahali hapo. Na watu wengi walimfuata naye akawaponya wote. 16 Akawa kataza wasimtangaze. 17 Hii ilikuwa ili yatimie maneno aliyosema nabii Isaya: 18 “Mtazameni mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu ambaye moyo wangu unapendezwa naye. Nitaweka Roho yangu juu yake , naye atatangaza haki kwa watu wa mataifa. 19 Hatabishana wala hatapiga kelele, sauti yake haitasikika mitaani. 20 Hataponda unyasi uliochubuliwa wala hatazima mshumaa unaokaribia kuzima, mpaka atakapoifanya haki ipate ushindi; 21 na watu wa mataifa wataweka tumaini lao katika jina lake.”

Yesu Na Beelzebuli

22 Kisha wakamletea kipofu mmoja ambaye pia alikuwa bubu na amepagawa na pepo. Yesu akamponya akaweza kusema na kuona. 23 Watu wote wakashangaa wakaulizana, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?” 24 Lakini Mafarisayo waliposikia haya wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mfalme wa pepo wote.”

25 Yesu alifahamu mawazo yao, akawaambia, “Utawala wo wote ambao umegawanyika wenyewe kwa wenyewe utaanguka. Hali kadhalika mji wo wote au jamaa ye yote iliyogawanyika yenyewe kwa yenyewe haitadumu. 26 Na kama shetani anamfukuza shetani, atakuwa amega wanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utaendeleaje? 27 Na kama mimi hutoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, watu wenu je, wao hutoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao ndio watakaowaamulia. 28 Lakini kama ninatoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia. 29 Au inawezekanaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang’anya mali yake yote pasipo kwanza kumfunga yule mwenye nguvu? Akisha mfunga ndipo hakika anaweza kupora mali yake.

30 “Mtu asiyekuwa pamoja nami ananipinga; na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, anatawanya. 31 Kwa hiyo nawaambieni, watu watasamehewa kila aina ya dhambi na kufuru lakini mtu ata kayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.

32 “Na mtu atakayesema neno kumpinga Mwana wa Adamu ata samehewa, lakini ye yote atakayempinga Roho Mtakatifu hatasame hewa, katika ulimwengu huu wala katika ulimwengu ujao.”

Maneno Huonyesha Hali Ya Moyo

33 “Ili upate matunda mazuri lazima uwe na mti mzuri; ukiwa na mti mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulikana kwa matunda yake. 34 Ninyi uzao wa nyoka! Mnawe zaje kunena mema wakati ninyi ni waovu? Kwa maana mtu husema yaliyojaa moyoni mwake. 35 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutokana na hazina ya wema uliohifadhiwa ndani yake; na mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutokana na hazina ya uovu uliohifadhiwa ndani yake.

36 “Nawaambia hakika, siku ya hukumu watu watatakiwa kujieleza kuhusu kila neno lisilo la maana walilolisema. 37 Kwa maana kutokana na maneno yako utahesabiwa haki, na kutokana na maneno yako utahukumiwa.”

Ishara Ya Yona

38 Kisha baadhi ya waandishi wa sheria na Mafarisayo wakam wambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” 39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi cha watu waovu na wasiowaami nifu hutafuta ishara; lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi. 41 Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu wakati Yona alipowahubiria, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki; kwa kuwa yeye alisafiri kutoka miisho ya dunia ili akaisikilize hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.”

Mafundisho Kuhusu Pepo Mchafu

43 “Pepo mchafu akimtoka mtu, huzunguka sehemu kame akita futa mahali pa kupumzika, lakini hapati. 44 Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye ile nyumba yangu nilikotoka.’ Na anaporudi, anaikuta ile nyumba ikiwa tupu, imefagiliwa na kupangwa vizuri. 45 Kisha huenda na kuwaleta pepo wengine saba, wabaya zaidi kuliko yeye, nao huingia na kuishi huko. Na hali ya mwisho ya mtu huyo inakuwa mbaya zaidi kuliko mwanzo.”

Ndugu Wa Yesu

46 Wakati alipokuwa akizungumza na watu, mama yake na ndugu zake walisimama nje wakataka kuongea naye. [ 47 Mtu mmoja akam wambia, “Mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kuon gea na wewe.”] 48 Lakini akamjibu yule mtu aliyemwambia, “Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni nani?” 49 Akinyoosha kidole chake kwa wanafunzi wake, alisema , “Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu! 50 Kwa maana ye yote anayefanya mapenzi ya Baba yangu wa mbinguni, ndiye kaka, dada na mama yangu.”

Mfano Wa Mbegu

13 Siku hiyo hiyo Yesu alitoka nyumbani akaketi kando ya bahari. Umati mkubwa mno wa watu wakasongamana hata ikabidi aingie katika mashua akaketi humo; na wale watu wakakaa ukingoni mwa bahari. Kisha akawaambia mambo mengi kwa mifano, akasema: “Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. Alipokuwa akitawanya mbegu, baadhi zikaanguka njiani, ndege wakaja wakazila. Nyingine zikaanguka kwenye mawe, ambapo hapakuwa na udongo wa kutosha. Zikakua haraka kwa sababu udongo ulikuwa kidogo. Lakini jua kali lilipowaka, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikwenda chini. Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba. Miiba hiyo ikakua ikazisonga. Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri zikatoa mazao, nyingine mara mia moja zaidi ya mbegu zilizopandwa, nyingine mara sitini na nyingine mara the lathini. Mwenye nia ya kusikia na asikie.”

Sababu Ya Kufundisha Kwa Mifano

10 Wanafunzi wake wakamwendea wakamwuliza, “Kwa nini unazungumza na watu kwa mifano?” 11 Akawajibu, “Ninyi mmejal iwa kuzifahamu siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujal iwa. 12 Kwa maana mtu aliye na kitu ataongezewa mpaka awe navyo tele; lakini mtu asiye na kitu, hata kile alichonacho atany ang’anywa. 13 Hii ndio sababu nazungumza nao kwa mifano; wanata zama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawae lewi. 14 Hali yao inatimiza ule utabiri wa nabii Isaya ali posema:’Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa, na pia mtatazama lakini hamtaona. 15 Kwa maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kuelewa kwa mioyo yao, wakanigeukia, nami nikawaponya.’ 16 Lakini macho yenu yame barikiwa, kwa maana yanaona, na masikio yenu yamebarikiwa kwa maana yanasikia. 17 Nawaambieni kweli, manabii wengi na wenye haki walitamani kuona mnayoyaona, na hawakuyaona; na kusikia mnayosikia lakini hawakuyasikia.”

Maelezo Ya Mfano Wa Mbegu

18 “Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi aliyepanda mbegu. 19 Mtu anaposikia neno la Ufalme na asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake; hii ndio mbegu iliyopandwa njiani. 20 Mbegu iliyopandwa kwenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na kulipokea mara moja kwa furaha. 21 Lakini kwa kuwa hana mizizi ndani yake, neno hilo hukaa kwa muda mfupi; na inapotokea dhiki au mateso kwa ajili ya hilo neno, yeye mara moja huanguka. 22 Mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno na mahangaiko ya maisha haya na anasa za mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda. 23 Lakini mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika huzaa matunda, mara mia, au mara sitini, au mara thelathini zaidi ya mbegu iliyo pandwa.”

Mfano Wa Magugu

24 Yesu akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa mbi nguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. 25 Lakini watu walipokuwa wamelala, adui yake aka ja akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26 Ngano ilipoota na kuzaa, magugu nayo yakachipua.

27 “Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwul iza, ‘Bwana, si ulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Imekuwaje kuna magugu?’ 28 Akawajibu, ‘Adui ndiye amefanya jambo hili’. Wale watumishi wakamwuliza, ‘Sasa unataka tukayang’oe?’ 29 Lakini akasema, ‘Hapana msiyang’oe, kwa maana huenda katika kung’oa magugu mkang’oa na ngano pia. 30 Acheni ngano na magugu yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavu naji wayang’oe magugu kwanza wayafunge katika mafurushi tayari kwa kuchomwa moto, lakini wavune ngano na kuikusanya ghalani mwangu.’ ”

Mfano Wa Haradali

31 Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa mbinguni unafanana na punje ndogo ya haradali ambayo mtu aliichukua akaipa nda shambani mwake. 32 Ijapokuwa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua, mmea wake huwa mkubwa kuliko mimea yote bustanini; nao huwa mti mkubwa ambao ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”

Mfano Wa Chachu

33 Akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika vipimo vitatu vya unga mpaka wote ukaumuka.”

Sababu Ya Yesu Kutumia Mifano

34 Haya yote Yesu aliwaeleza umati wa watu kwa kutumia mifano. Na hakika hakuwaambia lo lote pasipo kutumia mfano. 35 Hii ilikuwa kutimiza utabiri wa nabii, kwamba, ‘Nitazungumza nao kwa mifano; nitatamka mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.’

Ufafanuzi Wa Mfano Wa Magugu

36 Kisha Yesu akaagana na huo umati wa watu, akaingia nyum bani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.”

37 Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni mimi Mwana wa Adamu. 38 Shamba ni ulimwengu, na mbegu nzuri ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu. 39 Yule adui aliyepanda magugu ni shetani. Mavuno ni mwisho wa ulimwengu; na wavunaji ni malaika. 40 Kama vile magugu yanavyong’olewa na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa ulimwengu. 41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika wake wang’oe kutoka katika Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote. 42 Nao wata watupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 43 Ndipo wenye haki watang’aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Mwenye nia ya kusikia, na asikie.”

Mfano Wa Hazina Iliyofichwa

44 “Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani ambayo mtu mmoja aliigundua akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akanu nua lile shamba.” 45 Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na mfanya biashara aliyekuwa akitafuta lulu safi, 46 ambaye alipo pata lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza vyote alivyo kuwa navyo akainunua.”

Mfano Wa Wavu

47 “Na tena Ufalme wa mbinguni ni kama wavu wa kuvulia samaki ambao ulitandazwa baharini ukakamata samaki wa kila aina. 48 Ulipojaa, wavuvi waliuvuta ukingoni, wakachagua samaki wazuri wakawaweka kwenye vyombo safi, lakini wale samaki wabaya wakawat upa.

49 “Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki. 50 Na watawatupa hao waovu katika tanuru ya moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 51 Je, mmeyaelewa haya yote?” Wakam jibu, “Ndio.” 52 Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka katika ghala yake mali mpya na mali ya zamani.”

Yesu Akataliwa Nazareti

53 Yesu alipomaliza kutoa mifano hii, aliondoka. 54 Alipo fika mji wa kwao, aliwafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza? 55 Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si anaitwa Mariamu, na ndugu zake ni Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake si wako hapa nasi? Amepata wapi basi mambo haya yote?” 57 Wakakataa kumpokea. Lakini Yesu aka waambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake na nyumbani kwake.”

58 Na hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.

Yohana Mbatizaji Akatwa Kichwa

14 Wakati huo, mfalme Herode alisikia habari za Yesu; akawaam bia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji, amefufuka kutoka kwa wafu; ndio sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumweka gere zani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, kaka yake. Kisa che nyewe ni kwamba Yohana alikuwa amemwambia Herode kuwa, “Si halali kwako kumwoa huyo mwanamke.” Herode alitaka sana kumwua Yohana lakini akaogopa watu kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. Lakini siku ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya watu walioalikwa akamfurahisha sana Herode. Naye akaahidi kwa kiapo kumpa huyo binti lo lote atakaloomba. Kwa kushawishiwa na mama yake, huyo binti akasema, “Nipatie kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” Mfalme akajuta; lakini kwa ajili ya kile kiapo alichoapa mbele ya wageni, aliamuru kwamba ombi lake litekelezwe. 10 Akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani, 11 na kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.

12 Wanafunzi wa Yohana wakaja, wakauchukua mwili wake wakau zika. Kisha wakaenda, wakamwambia Yesu.

Yesu Alisha Zaidi Ya Watu Elfu Tano

13 Yesu aliposikia haya, aliondoka kwa mashua akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu wal ipata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu, kutoka mij ini. 14 Yesu alipofika kando ya bahari aliona umati mkubwa wa watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.

15 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walimfuata wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na siku imekwisha. Waage watu waondoke ili wakajinunulie chakula vijijini.” 16 Yesu akasema, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.” 17 Wakamjibu, “Hapa tuna mikate mitano na samaki wawili tu.” 18 Akawaambia, “Leteni hapa.” 19 Akaagiza wale watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akaibariki. Akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 20 Wote wakala, wakatosheka. Na wanafunzi wake wakakusanya vipande vipande vilivyosalia, waka jaza vikapu kumi na viwili. 21 Idadi ya watu waliokula, bila kuhesabu wanawake na watoto, ilikuwa kama wanaume elfu tano.

Yesu Atembea Juu Ya Maji

22 Baadaye Yesu akawaambia wanafunzi wake watangulie kwe nye mashua waende ng’ambo ya pili ya ziwa, wakati yeye anawaaga wale watu. 23 Baada ya kuwaaga, akaenda mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa hapo peke yake. 24 Wakati huo ile mashua ilikwisha fika mbali, ikisukwa sukwa na mawimbi kwa sababu upepo ulikuwa mkali.

25 Ilipokaribia alfajiri, Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26 Lakini wanafunzi wake walipom wona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu. Wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga mayowe kwa hofu. 27 Lakini mara moja Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo. Ni mimi; msiogope.”

28 Petro akamjibu, “Bwana, kama ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.” 29 Yesu akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka katika mashua, akatembea juu ya maji akimfuata Yesu. 30 Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”

31 Mara Yesu akanyoosha mkono wake, akamshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini ulikuwa na shaka?” 32 Na walipoingia katika mashua, upepo ukakoma. 33 Wote waliokuwamo katika mashua wakamwabudu wakisema, “Hakika, wewe ni Mwana wa

Yesu Awaponya Wagonjwa Genesareti

34 Walipokwisha kuvuka, wakafika Genesareti. 35 Watu wa eneo lile walipomtambua Yesu, walipeleka habari sehemu zote za jirani na watu wakawaleta wagonjwa wote kwake 36 wakamsihi awaru husu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa, waliponywa.

Mafundisho Ya Mafarisayo

15 Baadhi ya walimu wa sheria na Mafarisayo kutoka Yerusalemu walikuja kwa Yesu wakamwuliza, “Mbona wanafunzi wako hawafu ati mafundisho ya wazee wetu? Kwa maana wao hawanawi mikono ka bla ya kula!” Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnazivunja amri za Mungu kwa ajili ya mafundisho yenu? Kwa maana Mungu alisema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako’ na ‘Ye yote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ Lakini ninyi mnasema kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kuku saidia nacho nimekitoa kwa Mungu,’ basi hana wajibu tena wa kum saidia baba yake. Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. Ninyi wanafiki! Isaya alisema sawa juu yenu alipotabiri kwamba: ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Kuniabudu kwao ni bure, na mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu.’ ”

Usafi Wa Kweli

10 Yesu akaita ule umati wa watu akawaambia, “Sikilizeni kwa makini na mwelewe: 11 kinachomfanya mtu kuwa mchafu mbele ya Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.” 12 Kisha wanafunzi wake wakaja wakamwambia, “Unafahamu kwamba Mafarisayo walichukizwa sana na yale maneno uliyosema?”

13 Akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hakuupanda, utang’olewa. 14 Waacheni; wao ni viongozi vipofu. Na kama kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, wote wawili watatumbukia shimoni.”

15 Petro akasema, “Tuambie maana ya mfano huo.” 16 Yesu akawauliza, “Hata na ninyi bado hamwelewi? 17 Hamtambui kwamba cho chote kiingiacho mdomoni hupitia tumboni na hatimaye hutolewa nje? 18 Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kinachomfanya mtu kuwa mchafu. 19 Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo machafu, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na matukano. 20 Haya ndio yamchafuayo mtu, lakini kula bila kunawa mikono hakumchafui mtu.”

21 Na Yesu akaondoka mahali hapo akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. 22 Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu hizo akaja kwake, akamlilia, akasema, “Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa na pepo na anasumbuka sana.” 23 Lakini Yesu hakumjibu neno. Basi wanafunzi wake wakamwendea wakamwomba, “Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele. ” 24 Akajibu, “Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli wal iopotea.”

25 Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Yesu akasema, “Bwana, nisaidie!” 26 Yesu akajibu, “Si haki kuchu kua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” 27 Yule mwanamke akajibu, “Ndio, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoan guka kutoka kwenye meza za mabwana wao.”

28 Ndipo Yesu akamwambia, “Mama, imani yako ni kubwa! Na ufanyiwe kama unavyotaka.” Tangu wakati huo mtoto wake akapona.

Yesu Aponya Watu Wengi

29 Yesu akaondoka mahali hapo akapita kando ya bahari ya Galilaya. Akapanda mlimani, akaketi huko . 30 Umati mkubwa wa watu wakamjia wakiwaleta viwete, vilema, vipofu, viziwi na wen gine wengi, wakawaweka karibu yake; naye akawaponya. 31 Watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Yesu Alisha Watu Elfu Nne

32 Kisha Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Nina waonea huruma watu hawa kwa maana wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu sasa na hawana chakula. Sipendi kuwaaga wakiwa na njaa wasije wakazimia njiani.”

33 Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi chakula cha kutosha kuwalisha watu hawa wote, nasi tuko nyikani?” 34 Na Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakamjibu, “Saba, na samaki wadogo wachache.” 35 Yesu akaamuru watu wakae chini. 36 Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, akamshukuru Mungu, akavimega akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 37 Wote wakala, wakashiba. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. 38 Idadi ya watu waliokula ilikuwa elfu nne bila kuhesabu wanawake na watoto.

39 Baada ya kuwaaga watu, Yesu akaingia katika mashua akaenda sehemu za Magadani.

Mafarisayo Wadai Ishara

16 Mafarisayo na Masadukayo walikuja kwa Yesu, wakiwa na nia ya kumtega. Kwa hiyo wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbin guni. Akawajibu, “Ifikapo jioni mnasema, ‘Kwa kuwa anga ni nyekundu, hali ya hewa itakuwa nzuri.’ Na asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na mvua kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yame tanda.’ Mnajua jinsi ya kusoma dalili za anga, lakini hamwezi kutambua dalili za nyakati. Kizazi cha waovu na watu wasio waaminifu hutafuta ishara. Lakini hakitapewa ishara yo yote isi pokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake.

Chachu Ya Mafarisayo Na Masadukayo

Walipokwisha kuvuka hadi ng’ambo ya pili ya ziwa, wanafunzi wake waligundua kuwa walisahau kuchukua mikate. Yesu akawaam bia, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.” Wakabishana kati yao wakisema, “Ni kwa sababu hatukuleta mikate.”

Lakini Yesu, akitambua mazungumzo yao, alisema, “Enyi watu wenye imani haba! Mbona mnajadiliana kuhusu kutokuwa na mikate? Bado tu hamwelewi? Hamkumbuki ile mikate mitano iliyolisha watu elfu tano na idadi ya vikapu vya mabaki mlivyokusanya? 10 Au ile mikate saba iliyolisha watu elfu nne na idadi ya vikapu vya mabaki mlivyokusanya? 11 Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sizungumzii habari za mikate? Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” 12 Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hazungumzii juu ya hamira ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ni Mwana Wa Mungu

13 Basi Yesu alipofika katika wilaya ya Kaisaria Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, “Watu husema mimi Mwana wa Adamu kuwa ni nani?” 14 Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya; na wengine husema kwamba ni Yeremia au mmo jawapo wa manabii.” 15 Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani? 16 Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”

Mwana wa Mungu aliye hai.”

17 Na Yesu akamwambia, “Umebarikiwa, Simoni mwana wa Yona, kwa maana si mwanadamu aliyekufunulia hili, bali ni Baba yangu aliye mbinguni. 18 “Nami nakuambia, wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo hata nguvu za kuzimu haziwezi kulishinda. 19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni na lo lo te utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lo lote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”

20 Kisha akawakataza wasimwambie mtu ye yote kwamba yeye ndiye Kristo.

Yesu Anazungumza Juu Ya Mateso Yake

21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi kutoka kwa wazee, makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na siku ya tatu atafufuliwa.

22 Petro akamchukua kando akaanza kumkemea akamwambia, “Mungu apishie hayo mbali! Jambo hili halitakupata kamwe!” 23 Lakini Yesu akageuka akamwambia Petro , “Toka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo hayo si ya Mungu bali ya binadamu.”

24 Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu akitaka kuni fuata, ni lazima ajikane mwenyewe na achukue msalaba wake, anifu ate. 25 Kwa maana mtu akitaka kuokoa nafsi yake, ataipoteza; lakini mtu atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataipata tena.

26 “Kwa maana mtu atapata faida gani akiupata ulimwengu wote lakini akaipoteza nafsi yake? Au mtu atabadilisha nini na nafsi yake? 27 Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nitakuja katika utukufu wa Baba yangu pamoja na malaika wangu na nitamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 28 Nawaambieni kweli, baadhi yenu hapa hawataonja kifo kabla ya kuniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika Ufalme wangu.”

Yesu Abadilika Sura Mlimani

17 Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake Yakobo, wakaenda peke yao juu ya mlima mrefu. Na wakiwa huko, Yesu akabadilika sura mbele yao, uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa nyeupe kama mwanga. Na mara Musa na Eliya wakawatokea, wakawa wakizungumza na Yesu. Kisha Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri kwamba sisi tuko hapa. Ukiniruhusu, nitatengeneza vibanda vitatu hapa: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Eliya.”

Petro alipokuwa bado akizungumza, ghafla, wingu linalong’aa likatanda juu yao na sauti ikatoka kwenye wingu hilo ikasema, “Huyu ni mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa naye; msikilizeni yeye.” Wanafunzi waliposikia haya walianguka chini kifudifudi wakajawa na hofu. Lakini Yesu akaja, akawagusa, akawaambia, “Inukeni. Msiogope.” Walipoinua macho yao hawakumwona mtu mwingine isipokuwa Yesu peke yake.

Walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaambia, “Msimwambie mtu ye yote maono haya mpaka mimi Mwana wa Adamu nitakapofufuliwa kutoka kwa wafu.”