Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake

27 Wakafika tena Yerusalemu. Wakati Yesu alipokuwa akitem bea Hekaluni, makuhani wakuu, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia 28 wakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?

Na ni nani aliyekupa mamlaka hayo?”

29 Yesu akawajibu, “Nitawauliza swali mmoja. Mkinijibu, mimi pia nitawaeleza ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 30 Niambieni, mamlaka aliyotumia Yohana kubatiza watu, yalitoka kwa Mungu au kwa watu?”

31 Wakaanza kubishana, “Tukisema, ‘Yalitoka kwa Mungu’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 32 Je, tunaweza kusema ‘Yali toka kwa watu’? - Waliogopa watu kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa nabii. 33 Kwa hiyo wakamjibu, “Hatujui.” Na Yesu akawaambia, “Mimi pia sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”

Read full chapter

Viongozi Wawa na Mashaka Kuhusu Mamlaka ya Yesu

(Mt 21:23-27; Lk 20:1-8)

27 Yesu na wanafunzi wake walirudi Yerusalemu. Na walipokuwa wakitembea ndani ya viwanja vya Hekalu, viongozi wa makuhani, walimu wa Sheria na wazee walimjia Yesu 28 na kumwuliza, “Kwa mamlaka gani unafanya vitu hivi? Nani alikupa mamlaka ya kuvifanya?”

29 Yesu akawaambia, “Nitawauliza swali, na mkinijibu, ndipo nitawaeleza kwa mamlaka gani ninafanya vitu hivi. 30 Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni ama ulitoka kwa watu? Sasa mnijibu basi.”

31 Walijadiliana wao kwa wao wakisema, “Tukisema ‘ulitoka mbinguni’, atasema, ‘Kwa nini basi hamumuamini?’ 32 Lakini kama tukisema kuwa ubatizo wa Yohana ulitoka kwa wanadamu, watu watatukasirikia.” Viongozi waliwaogopa watu, kwani watu wote waliamini kuwa Yohana kweli alikuwa nabii.

33 Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Hatufahamu.”

Hivyo Yesu akawaambia, “Hata mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nafanya mambo haya.”

Read full chapter