Luka 19:1-23:46
Neno: Bibilia Takatifu
19 1 Yesu akaingia Yeriko, akiwa safarini kuelekea Yerusalemu. 2 Hapo, alikuwapo mtu mmoja mkuu wa watoza kodi na pia mtu tajiri, jina lake Zakayo. 3 Yeye alitamani sana kumwona Yesu lakini hakuweza kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, naye alikuwa mfupi sana. 4 Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati akapanda juu ya mkuyu ili amwone Yesu ambaye angepitia njia ile. 5 Yesu alipofika chini ya huo mkuyu, akatazama juu akamwambia: “Zakayo! Shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani kwako!” 6 Mara moja Zakayo akashuka, akamkaribisha Yesu nyumbani kwake kwa furaha kubwa. 7 Watu wote waliokuwepo, wakaanza kunung’unika, “Amekwenda kuwa mgeni nyumbani kwa mwenye dhambi!” 8 Lakini Zakayo akasimama akamwambia Bwana, “Sikia Bwana, nusu ya mali yangu ninaitoa hivi sasa niwagawie maskini, na kama nimemdhulumu mtu ye yote, nitamrudishia mara nne zaidi.” 9 Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumba hii, kwa sababu huyu naye ni mtoto wa Ibrahimu. 10 Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nimekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”
Mfano Wa Fedha
11 Wakati walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu aliendelea kuwaambia mfano. Wakati huo watu walikuwa wakidhani kwamba kwa kuwa walikuwa wanakaribia Yerusalemu, Ufalme wa Mungu ungetokea mara. 12 Kwa hiyo akawaambia: “Mtu mmoja wa ukoo wa kitawala, alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi. 13 Akawaita watumishi wake kumi akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Zitumieni kufanyia biash ara mpaka nitakaporudi.’ 14 Lakini raia wake walimchukia wakapeleka ujumbe usemao, ‘Hatutaki huyu mtu awe mfalme wetu. ’ 15 Hata hivyo alipewa ufalme akarudi nyumbani. Kisha akawaita wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha, ili afahamu faida kila mmoja wao aliyopata.
16 “Wa kwanza akaja, akasema, ‘Bwana, kutokana na fedha uliyoniachia nimepata faida mara kumi zaidi.’ 17 Yule bwana akamjibu, ‘Umefanya vizuri mtumishi mwema! Kwa sababu umekuwa mwaminifu katika wajibu mdogo sana, nakupa mamlaka juu ya miji kumi.’
18 “Wa pili naye akaja, akasema, ‘Bwana, fedha yako imeleta faida mara tano zaidi.’ 19 Bwana wake akajibu, ‘Nakupa mamlaka juu ya miji mitano.’ 20 Kisha akaja mtumishi mwingine akasema, ‘Bwana hii hapa fedha yako. Niliitunza vizuri kwenye kitambaa. 21 Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unachukua ambapo hukuweka kitu na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’
22 “Bwana wake akamjibu, ‘Nitakuhukumu kwa maneno yako mwe nyewe, wewe mtumishi mwovu ! Kama ulifahamu kwamba mimi ni mtu mkali, nichukuaye mahali ambapo sikuweka kitu na kuvuna ambapo sikupanda; 23 kwa nini basi hukuweka fedha zangu benki ili nita kaporudi nizichukue na faida yake?’ 24 Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu , ‘Mnyang’anyeni fungu lake la fedha mkampe yule mwenye kumi.’ 25 Wakamwambia, ‘Bwana, mbona tayari anayo mafungu kumi’? 26 Akajibu, ‘Nawahakikishieni kwamba, kila aliye na kitu, Mungu atamwongezea; na yule asiyetumia alicho nacho, atanyang’anywa hata hicho alicho nacho. 27 Sasa nileteeni wale maadui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme wao; waleteni hapa muwaue mbele yangu.”’
Yesu Aingia Yerusalemu
28 Alipokwisha kusema haya, Yesu alikaa mbele ya msafara akielekea Yerusalemu. 29 Na alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima wa Mizeituni aliwatuma wanafunzi wawili akawaagiza hivi, 30 “Nendeni katika kijiji kile kilicho mbele yenu. Mtaka pokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda ambaye hajapandwa na mtu bado, amefungwa. Mfungueni, mumlete hapa. 31 Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.”’
32 Wale waliotumwa wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. 33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana- punda wenyewe wakawauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?” 34 Wale wanafunzi wakajibu, “Bwana anamhitaji.” 35 Wakamleta kwa Yesu. Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, kisha wakampandisha Yesu juu yake. 36 Alipokuwa akienda, watu wakatan daza nguo zao barabarani. 37 Alipokaribia mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote wa wanafunzi wake wakaanza kwa sauti kuu kumsifu Mungu kwa furaha kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona Yesu akifanya, 38 wakasema: “Amebarikiwa Mfalme anayekuja kwa jina la Bwana! Amani mbinguni na Utukufu kwa Mungu.” 39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwemo katika umati wakamwambia, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako.” 40 Yesu akawajibu, “Nawaambia, hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele.”
Yesu Anaulilia Mji Wa Yerusalemu
41 Alipokaribia Yerusalemu, akauona mji, aliulilia,
42 akasema, “Laiti ungalijua leo jinsi ya kupata amani! Lakini sasa huoni! 43 Kuna siku ambapo maadui zako watakuzungushia ukuta na kukuzingira na kukushambulia kutoka kila upande. 44 Watakutupa chini wewe na wanao ndani ya kuta zako na hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine. Hii ni kwa sababu hukutaka kutambua wakati
Yesu Aingia Hekaluni
45 Ndipo akaingia Hekaluni akaanza kuwafukuza wale wal iokuwa wakifanya biashara humo. 46 Akawaambia, “Imeandikwa katika Maandiko, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala.’ Lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang’anyi.”
47 Kila siku alikuwa akifundisha Hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakiungwa mkono na viongozi wengine walijaribu kila njia wapate kumwua 48 lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote waliomfuata waliyasikiliza maneno yake kwa makini na kuyazingatia. Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake
20 Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, wakuu wa makuhani, walimu wa sheria na wazee walifika Hekaluni 2 wakamwuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?”
3 Akawajibu, “Na mimi nitawauliza swali. 4 Je, mamlaka ya Yohana ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa wanadamu? ” 5 Wakaanza kubishana wao kwa wao wakisema, “Tukisema, ‘Kwa Mungu’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 6 Na tukisema ‘Kwa wana damu,’ watu wote watatupiga mawe kwa sababu wanaamini kabisa kwamba Yohana alikuwa nabii.” 7 Basi wakajibu, “Hatujui mamlaka yake yalitoka wapi.” 8 Yesu akawaambia, “Na mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.’ ’
Mfano Wa Shamba La Mizabibu Na Wakulima
9 Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda mizabibu katika shamba lake, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu. 10 Wakati wa mavuno akamtuma mtumishi kwa hao wakulima aliowakodisha shamba ili wampatie sehemu ya mavuno. Lakini wale wakulima wakampiga na kumfukuza mikono mitupu. 11 Akamtuma mtumishi mwingine; naye pia wakam piga, wakamfanyia mambo ya aibu na kumfukuza. 12 Akampeleka wa tatu; wakamjeruhi na kumtupa nje ya shamba.
13 “Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu nimpendaye, bila shaka yeye watamhesh imu.’ 14 Lakini wale wakulima walipomwona, wakashauriana, ‘Huyu ndiye mrithi, hebu tumwue ili sisi turithi hili shamba.’ 15 Kwa hiyo wakamtoa nje ya shamba, wakamwua.” Ndipo Yesu akauliza, “Sasa yule mwenye shamba atawafanyia nini wakulima hawa?
16 Atakuja awaue awapatie watu wengine shamba hilo.” Watu waliposikia hayo wakasema, “Jambo hili lisi tokee!”
17 Lakini Yesu akawakazia macho akasema, “Basi ni nini maana ya maandiko haya, ‘Lile jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe la msingi.’
18 “Kila aangukaye kwenye jiwe hilo atakatika vipande vipande, na ye yote ambaye litamwangukia atasagika sagika.”
19 Waalimu wa sheria na wakuu wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja kwa sababu walifahamu kwamba huo mfano aliou toa uliwahusu wao. Lakini waliwaogopa watu.
Kuhusu Kulipa Kodi
20 Kwa hiyo wakawa wanamvizia. Wakawatuma wapelelezi wal iojifanya kuwa wana nia njema ya kujifunza. Walitumaini kumtega kwa maswali ili wamkamate kwa lo lote atakalosema, walitumie kumshtaki kwa Gavana. 21 Wale wapelelezi wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba maneno yako na mafundisho yako ni ya haki, kwamba huna upendeleo, na kwamba unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. 22 Je, sheria ya Musa inaturuhusu au haituruhusu kulipa kodi kwa
Kaisari?”
23 Lakini Yesu akatambua kwamba wanamtega, kwa hiyo akawaam bia, 24 “Nionyesheni sarafu ya fedha. Je, picha hii na maand ishi haya ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” 25 Aka waambia, “Basi, mpeni Kaisari vilivyo vyake na mpeni Mungu vil ivyo vyake.” 26 Wakashindwa kumkamata kwa maneno aliyosema mbele ya watu. Jibu lake liliwashangaza mno, wakakosa la kusema. Yesu Afundisha Kuhusu Ufufuo
27 Baadhi ya Masadukayo , wale wanaosema kwamba hakuna ufu fuo wa wafu, wakamjia Yesu wakamwuliza, 28 “Mwalimu, katika sheria ya Musa , tunasoma kwamba kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi kaka yake amwoe huyo mjane ili amzalie marehemu watoto. 29 Walikuwepo ndugu saba. Wa kwanza akafa bila kuzaa mtoto. 30 Kaka wa pili akamwoa huyo mjane 31 na wa tatu pia. Ikawa hivyo mpaka ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mama na wote wakafa pasipo kupata mtoto. 32 Mwishowe mama huyo naye akafa. 33 Je, siku ya ufufuo, mwanamke huyo ambaye aliolewa na wote saba atahesabiwa kuwa ni mke wa nani?”
34 Yesu akawajibu , “Katika maisha haya watu huoa na kuol ewa, 35 lakini wale ambao Mungu atawaona wanastahili kufufuka kutoka kwa wafu, watakapofika mbinguni hawataoa au kuolewa. 36 Hawa hawawezi kufa tena kwa sababu wao ni kama malaika; wao ni wana wa Mungu kwa kuwa wamefufuka kutoka kwa wafu. 37 Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka. Alimwita Bwana, ‘Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo,’ wakati Mungu aliposema naye katika kile kichaka kilichokuwa kikiwaka bila kuungua. 38 Yeye ni Mungu wa watu walio hai na si Mungu wa wafu kwa sababu kwa Mungu watu wote ni hai.” 39 Baadhi ya walimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umesema sawa kabisa!” 40 Na hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.
Uhusiano Kati Ya Kristo Na Daudi
41 Kisha akawaambia, “Inakuwaje watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 42 Maana Daudi mwenyewe katika kitabu cha Zaburi anasema, ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: kaa kulia kwangu 43 mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’
44 Sasa ikiwa Daudi anamwita Kristo ‘Bwana
Yesu Aonya Kuhusu Walimu Wa Sheria
45 Watu wote walipokuwa wakimsikiliza, Yesu akawaambia wana funzi wake, 46 “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa kanzu ndefu na kuamkiwa kwa heshima maso koni. Wao huchagua viti vya mbele katika masinagogi na kukaa kwe nye sehemu za wageni rasmi katika sherehe. 47 Wanawadhulumu wajane mali zao na kisha wanasali sala ndefu ili waonekane wao ni watu wema. Mungu atawaadhibu vikali zaidi kwa ajili ya haya.” Sadaka Ya Mjane
21 Alipokuwa Hekaluni Yesu aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la sadaka. 2 Akamwona na mama mmoja mjane, maskini sana, akiweka humo sarafu mbili. 3 Akasema, “Nawaambia kweli, huyu mjane ametoa sadaka kubwa zaidi kuliko hao wengine wote. 4 Kwa maana hao wengine wametoa sehemu ndogo tu ya utajiri wao, lakini yeye, ingawa ni maskini, ametoa vyote alivyokuwa navyo.”
Dalili Za Siku Za Mwisho
5 Baadhi ya watu walikuwa wakizungumza kuhusu Hekalu jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na mapambo maridadi yaliyotolewa kama sadaka kwa Mungu. Yesu akawaambia, 6 “Wakati unakuja ambapo vyote hivyo mnavyovistaajabia sasa vitabomolewa, halitabaki hata jiwe moja juu ya jingine.” 7 Wakamwuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini na ni dalili gani zitaonyesha kwamba yanakari bia?” 8 Akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja wakitumia jina langu, na kusema, ‘Mimi ndiye’ na ‘Wakati umekaribia’. Msiwafuate. 9 Na mtakaposikia habari za vita na machafuko, msiogope, kwa maana hayo ni lazima yatokee kwanza, ila mwisho hautatokea wakati huo.”
10 Kisha akawaambia: “Taifa moja litapigana na taifa lin gine na utawala mmoja utapigana na utawala mwingine. 11 Kutaku wepo na matetemeko ya ardhi, njaa kali na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali; kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.”
Mateso
12 “Lakini kabla haya yote hayajatokea watu watawakamata ninyi na kuwatesa. Mtashtakiwa mbele ya wakuu wa masinagogi na kufungwa magerezani; na wengine mtapelekwa kushtakiwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu. 13 Na hii itawapa nafasi ya kutoa ushuhuda kuhusu imani yenu. 14 Lakini msiwe na wasiwasi juu ya matayarisho ya utetezi wenu kabla ya mashtaka. 15 Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo maadui zenu hawa taweza kukataa au kupinga. 16 Mtasalitiwa na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na baadhi yenu mtauawa. 17 Watu wote watawa chukia kwa ajili yangu. 18 Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu! 19 Simameni imara nanyi mtaokoa nafsi zenu.”
Kuteketezwa Kwa Yerusalemu
20 “Mkiona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, faham uni kwamba karibu utaangamizwa. 21 Wakati huo, wale walio Yudea wakimbilie milimani; walio mjini Yerusalemu waondoke humo na wale walioko mashambani wasije mjini. 22 Kwa sababu huu utakuwa wakati wa kulipiza kisasi ili yale yote yaliyosemwa kwenye Maan diko yatimie.
23 “Ole wao akina mama watakaokuwa waja wazito na wata kaokuwa wakinyonyesha! Kutakuwa na dhiki nchini na ghadhabu ya Mungu itakuwa juu ya watu wa taifa hili. 24 Wengine watauawa kwa silaha na wengine watachukuliwa mateka na kupelekwa nchi mbalim bali. Na Yerusalemu itamilikiwa na watu wa mataifa mengine mpaka muda wa mataifa hayo utakapokwisha.”
Kuja Kwa Mwana Wa Adamu
25 “Kutakuwa na matukio ya ajabu kwenye jua, mwezi na nyota. Hapa ulimwenguni, mataifa yatakuwa katika dhiki na wasi wasi kutokana na ngurumo na dhoruba za kutisha zitakazotokea baharini. 26 Watu watakufa moyo kwa hofu na wasiwasi kuhusu yale wanayoogopa kuwa yataukumba ulimwengu; kwani nguvu za anga zita tikisika. 27 Ndipo wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika wingu kwa uwezo na utukufu mkuu. 28 Mambo haya yakianza kutokea, simameni imara, mjipe moyo, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.”
29 Akawaambia mfano, “Utazameni mtini na miti mingine yote. 30 Inapochipua majani, mnatambua ya kuwa wakati wa mavuno uko karibu. 31 Hali kadhalika, mkiyaona mambo haya yanatokea, faham uni kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia. 32 Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitakwisha kabla mambo haya hayajatokea. 33 Mbingu na nchi zitatoweka lakini maneno yangu yatadumu daima.” Siku Ya Mwisho Itakuja Ghafla
34 Jihadharini msije mkatawaliwa na ulafi, ulevi na wasiwasi wa maisha haya. Kisha siku ikafika pasipo ninyi kutazamia mka naswa! 35 Kwa maana siku hiyo itawakumba watu wote waishio duniani. 36 Kaeni macho na ombeni ili Mungu awawezeshe kuepuka yale yote yatakayotokea na mweze kusimama mbele yangu mimi Mwana wa Adamu.”
37 Kila siku Yesu alikuwa akifundisha Hekaluni na jioni ili pofika alikwenda kulala kwenye mlima wa Mizeituni. 38 Na asubuhi na mapema watu wote walikuwa wakija Hekaluni kumsikiliza.
22 Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ili kuwa imekaribia. 2 Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu kwa siri kwa sababu waliwaogopa watu.
3 Shetani akamwingia Yuda aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili. 4 Yuda akaenda kwa makuhani wakuu na wakubwa wa walinzi wa Hekalu akawaeleza jinsi ambavyo angeweza kumsaliti Yesu. 5 Wakafurahi na wakaahidi kumlipa fedha. 6 Naye akaridhika, akaanza kutafuta nafasi nzuri ya kumsaliti Yesu kwa siri. Maandalizi Ya Chakula Cha Pasaka
7 Ikafika siku ya Mikate isiyotiwa Chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. 8 Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.” 9 Wakam wuliza, “Tukaandae wapi?” 10 Akawajibu, “Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka kwenye nyumba atakayoingia, 11 kisha mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu anauliza, kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka? 12 Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani ambacho kina fanicha zote. Fanyeni maandalizi humo.”
13 Wakaenda wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaam bia. Kwa hiyo wakaandaa chakula cha Pasaka.
14 Wakati ulipofika Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 15 Kisha akawaambia “Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16 Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.” 17 Akapokea kikombe cha divai akashukuru, akasema, “Chukueni mnywe wote. 18 Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.”
19 Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.” 20 Vivyo hivyo baada ya kula, aka chukua kile kikombe cha divai akasema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu. 21 Lakini huyo atakayenisaliti amekaa nasi hapa mezani kama rafiki. 22 Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama ilivyokusudiwa na Mungu, lakini ole wake huyo mtu atakayenisaliti.” 23 Wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao angefanya kitu kama hicho.
Ubishi Kuhusu Ukubwa
24 Pia ukazuka ubishi kati ya wanafunzi kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa kati yao. 25 Yesu akawaambia, “Wafalme wa dunia huwatawala watu wao kwa mabavu na wenye mam laka huitwa ‘Wafadhili.’ 26 Ninyi msifanye hivyo. Aliye mkubwa wenu awe kama ndiye mdogo kabisa; na kiongozi wenu awe kama mtum ishi. 27 Kwani mkubwa ni nani? Yule aketiye mezani au yule anayemhudumia? Bila shaka ni yule aliyekaa mezani. Lakini mimi niko pamoja nanyi kama mtumishi wenu.
28 “Ninyi mmekuwa pamoja nami katika majaribu yangu: 29 na kama Baba yangu alivyonipa mamlaka ya kutawala; mimi nami nina wapa ninyi mamlaka hayo hayo. 30 Mtakula na kunywa katika karamu ya Ufalme wangu na kukaa katika viti vya enzi mkitawala makabila kumi na mawili ya Israeli.”
Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana
31 Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, shetani ameomba ruhusa kwa Mungu awapepete ninyi kama ngano. 32 Lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipotee. Na utakaponirudia mimi, uwatie moyo ndugu zako.”
33 Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda nawe gerezani na hata kufa.” 34 Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika leo usiku, utakana mara tatu kwamba hunijui.”
Kujiandaa Wakati Wa Hatari
35 Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma mwende bila mfuko, wala mkoba wala viatu, mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu, “La.” 36 Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko au mkoba auchukue. Asiye na upanga, auze koti lake anunue upanga. 37 Kwa sababu, nawambieni, yale Maandiko yaliyosema kwamba ‘Alihesabiwa pamoja na wahalifu’ yananihusu mimi na hayana budi kutimizwa. Naam, yale yaliyoandikwa kunihusu mimi yanatimia.” 38 Wakamwambia, “Bwana, tazama hapa kuna mapanga mawili.” Akawajibu, “Inatosha!. Yesu Asali Kwenye Mlima Wa Mizeituni
39 Ndipo Yesu akaondoka kuelekea kwenye mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, na wanafunzi wake wakamfuata. 40 Alipofika huko akawaambia wanafunzi, “Ombeni kwamba msiingie katika majaribu.” 41 Akaenda mbali kidogo nao, kama umbali anaoweza mtu kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 42 akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kwa mapenzi yangu, bali mapenzi yako yafanyike.” [ 43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44 Na alipokuwa katika uchungu mkubwa, akaomba kwa bidii zaidi na jasho lake likawa kama matone ya damu ikidondoka ardhini.] 45 Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wamechoka kwa huzuni. 46 Akawauliza, “Mbona mnalala? Amkeni muombe ili msiingie katika majaribu.”
Yesu Akamatwa
47 Wakati Yesu alipokuwa bado anazungumza, pakatokea kundi la watu likiongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wana funzi kumi na wawili. Akamsogelea Yesu ili ambusu. 48 Lakini Yesu akamwuliza, “Yuda! Unanisaliti mimi Mwana wa Adamu kwa busu?” 49 Wafuasi wa Yesu walipoona yanayotokea, wakasema, “Bwana, tutumie mapanga yetu?” 50 Na mmoja wao akampiga mtum ishi wa kuhani mkuu kwa panga, akamkata sikio la kulia. 51 Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa sikio la yule mtu, akamponya. 52 Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu na wakuu wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mme kuja na mapanga na marungu, kana kwamba mimi ni jambazi? 53 Kila siku nilikuwa pamoja nanyi lakini hamkunikamata. Lakini wakati huu, ambapo mtawala wa giza anafanya kazi, ndiyo saa yenu.”
Petro Amkana Yesu
54 Wakamkamata Yesu, wakamchukua wakaenda naye nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro akawafuata kwa mbali. 55 Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, na Petro akaketi na wale waliokuwa wakiota moto. 56 Msichana mmoja mfanyakazi akamwona Petro ameketi karibu na moto. Akamwangalia kwa makini, kisha akasema, “Huyu mtu pia ali kuwa pamoja na Yesu!” 57 Lakini Petro akakana akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” 58 Baadaye kidogo mtu mwingine akamwona Petro, akasema, “Wewe pia ni mmoja wao.” Petro akajibu, “Bwana, mimi si mmoja wao!” 59 Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akasisitiza, “Kwa hakika huyu mtu alikuwa na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.” 60 Petro akajibu, “Mimi sijui unalosema!” Na wakati huo huo, akiwa bado anazun gumza, jogoo akawika. 61 Yesu akageuka akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka yale maneno ambayo Bwana alimwambia, “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” 62 Akaenda nje, akalia kwa uchungu . Yesu Achekwa Na Kupigwa
63 Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64 Wakamfunga kitambaa usoni kisha wakasema, “Hebu nabii tuambie! Ni nani amekupiga?” 65 Wakamwambia maneno mengi ya kumtukana. Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza
66 Kulipokucha, Baraza la wazee wa Wayahudi, makuhani wakuu na walimu wa sheria wakakutana. Yesu akaletwa mbele yao. 67 Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, tuambie.” Yesu akawa jibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini, 68 na nikiwauliza swali, hamtanijibu. 69 Lakini hivi karibuni, mimi Mwana wa Adamu nita kaa upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi.” 70 Wote wakasema, “Ndio kusema wewe ndiye Mwana wa Mungu?” Akawajibu, “Ninyi ndio mmesema kwamba Mimi ndiye.” 71 Kisha wakasema, “Kwa nini tutafute ushahidi zaidi? Sisi wenyewe tumesikia maneno aliy osema.” Yesu Apelekwa Kwa Pilato
23 Wote waliokuwepo katika Baraza wakasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. 2 Wakafungua mashtaka yao kwa kusema: “Tumem wona huyu mtu akipotosha taifa letu. Yeye anawaambia watu wasi lipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.” 3 Basi Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamjibu, “Ni kama ulivyosema.” 4 Pilato akawaambia maku hani wakuu na watu wote waliokuwapo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki huyu mtu!” 5 Lakini wao wakakazana kusema, “Anawa chochea watu kwa mafundisho yake katika Yudea yote. Alianzia huko
Yesu Apelekwa Kwa Herode
6 Pilato aliposikia hayo akauliza, ‘Huyu mtu ni Mgalilaya?” 7 Alipofahamu kwamba Yesu alitoka katika mkoa unaotawaliwa na Herode, akampeleka kwa Herode ambaye wakati huo alikuwa Yerus alemu. 8 Herode alifurahi sana kumwona Yesu. Alikuwa amesikia habari zake na kwa muda mrefu akatamani sana kumwona; na pia alitegemea kumwona Yesu akifanya mwujiza. 9 Kwa hiyo akamwuliza Yesu maswali mengi, lakini yeye hakumjibu neno. 10 Wakati huo, makuhani wakuu na walimu wa sheria walikuwepo wakitoa mashtaka yao kwa nguvu sana. 11 Herode na maaskari wake wakamkashifu Yesu na kumzomea. Wakamvika vazi la kifahari, wakamrudisha kwa Pilato. 12 Siku hiyo, Herode na Pilato, ambao kabla ya hapo walikuwa maadui, wakawa marafiki.
Yesu Ahukumiwa Kifo
13 Pilato akawaita makuhani wakuu, viongozi na watu 14 aka waambia, “Mmemleta huyu mtu kwangu mkamshtaki kuwa anataka kuwa potosha watu. Nimemhoji mbele yenu, na sikuona kuwa ana hatia kutokana na mashtaka mliyoleta. 15 Hata Herode hakumwona na kosa lo lote; ndio sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lo lote linalostahili adhabu ya kifo. 16 Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko, kisha nimwachilie.” [ 17 Kwa kawaida, kila sikukuu ya Pasaka ilimlazimu Pilato kuwafungulia mfungwa mmoja].
18 Watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “ Auawe huyo! Tufungulie Baraba!” 19 Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini. 20 Pilato ali taka sana kumwachilia Yesu kwa hiyo akasema nao tena. 21 Lakini wao wakazidi kupiga kelele, “Msulubishe! Msulubishe!” 22 Kwa mara ya tatu Pilato akasema nao tena, “Amefanya kosa gani huyu mtu? Sioni sababu yo yote ya kutosha kumhukumu adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko kisha nimwachilie .”
23 Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu na kusisi tiza kwamba Yesu asulubiwe. Hatimaye, kelele zao zikashinda. 24 Pilato akaamua kutoa hukumu waliyoitaka. 25 Akamwachia huru yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini; akamkabidhi Yesu mikononi mwao, wamfa nyie watakavyo. Yesu Asulubiwa Msalabani
26 Na walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja ait waye Simoni wa Kirene aliyekuwa anatoka mashambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha atembee nyuma ya Yesu. 27 Umati mkubwa wa watu wakamfuata Yesu ikiwa ni pamoja na wanawake waliokuwa wakimlilia na kuomboleza. 28 Lakini Yesu akawageukia, akawaam bia, “Enyi akina mama wa Yerusalemu, msinililie mimi bali jilil ieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29 Kwa maana wakati utafika ambapo mtasema, ‘Wamebarikiwa akina mama tasa, ambao hawakuzaa na matiti yao hayakunyonyesha.’ 30 Na watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni’ na vilima, ‘Tufunikeni’. 31 Kwa maana kama watu wanafanya mambo haya wakati mti ni mbichi, itakuwaje utakapo kauka?”
32 Wahalifu wengine wawili pia walipelekwa wakasulubiwe pamoja na Yesu. 33 Walipofika mahali paitwapo “Fuvu la kichwa,” wakamsulubisha Yesu hapo pamoja na hao wahalifu; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.
34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui wali tendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. 35 Watu wakasi mama pale wakimwangalia. Viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Si aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama kweli yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.” 36 Askari nao wakam wendea, wakamdhihaki. Wakamletea siki anywe, 37 wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe tuone.”
38 Na maandishi haya yaliwekwa kwenye msalaba juu ya kichwa chake: “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.” 39 Mmoja kati ya wale wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”
40 Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa. 41 Adhabu yetu ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini huyu hakufanya kosa lo lote.” 42 Kisha akasema, “Bwana Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”
Yesu Afa Msalabani
44 Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa, 45 kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili. 46 Yesu akapaza sauti akasema, “Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.
Copyright © 1989 by Biblica