47 Kwa hiyo nakuambia, upendo mkubwa aliouonyesha huyu mama unathibitisha kuwa dhambi zake ambazo ni nyingi zimesamehewa. Lakini ye yote asamehewaye kidogo, huonyesha upendo kidogo.”

48 Akamwambia yule mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.” 49 Ndipo wale wageni wengine waliokuwepo wakaanza kuulizana, “Hivi huyu ni nani, hata aweze kusamehe dhambi?” 50 Yesu akam wambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”

Read full chapter

47 Ninakwambia kuwa dhambi zake zilizo nyingi zimesamehewa. Hii ni wazi, kwa sababu ameonesha upendo mkubwa. Watu wanaosamehewa kidogo hupenda kidogo.”

48 Kisha akamwambia mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.”

49 Watu waliokaa naye sehemu ya chakula wakaanza kusema mioyoni mwao, “Mtu huyu anadhani yeye ni nani? Anawezaje kusamehe dhambi?”

50 Yesu akamwambia mwanamke, “Kwa sababu uliamini, umeokolewa kutoka katika dhambi zako. Nenda kwa amani.”

Read full chapter