Msiambatane Na Wasioamini

14 Msiambatane pamoja na watu wasioamini. Kwa maana kuna uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 15 Kuna kuelewana gani kati ya Kristo na shetani? Mwamini ana uhusiano gani na asiyeamini? 16 Kuna uelewano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema, “Nitaishi ndani yao na kutembea kati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

Read full chapter