Add parallel Print Page Options

Lakini tumekataa mambo ya aibu ya siri. Hatumdanganyi mtu yeyote, na hatuyabadilii mafundisho ya Mungu. Tunaifundisha kweli wazi wazi. Na hivi ndivyo watu wanaweza kutambua mioyoni mwao sisi ni watu wa namna gani mbele za Mungu. Habari Njema tunazowahubiri watu hazijafichika kwa yeyote isipokuwa kwa waliopotea. Mtawala[a] wa dunia hii amezitia giza akili za wasioamini. Hawawezi kuona nuru ya Habari Njema; ujumbe juu ya uungu wa Kristo, taswira halisi ya Mungu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 4:4 Mtawala Kwa maana ya kawaida, “Mungu”. Lakini usemi huu hapa unamaanisha “Shetani”.