Yesu Na Beelzebuli

20 Yesu akarudi nyumbani. Umati wa watu ukamfuata tena, hata yeye na wanafunzi wake wakashindwa kula chakula. 21 Ndugu zake walipopata habari walikuja kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”

22 Walimu wa sheria waliotoka Yerusalemu walikuwa wakisema, “Amepagawa na Beelzebuli, mkuu wa mashetani; na ni kwa uwezo wa Beelzebuli anawafukuza mashetani.”

Beelzebuli anawafukuza mashetani.”

23 Basi Yesu akawaita akazungumza nao kwa mifano: “Shetani awezaje kufukuza shetani? 24 Ikiwa utawala wa nchi umegawanyika wenyewe, hauwezi kudumu. 25 Hali kadhalika kama jamaa moja ime gawanyika yenyewe kwa yenyewe, jamaa hiyo haiwezi kudumu. 26 Na kama shetani akijipiga vita yeye mwenyewe hatatimiza cho chote ila mwisho wake umekaribia. 27 Pia hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumwibia vitu vyake vyote pasipo kwanza kumfunga huyo mwenye nyumba mwenye nguvu. Akisha mfunga, ndipo anaweza kumwibia kila kitu.

Read full chapter