Marko 3:13-19
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yesu Achagua Wanafunzi Wake Kumi na Wawili
(Mt 10:1-4; Lk 6:12-16)
13 Kisha Yesu akapanda juu kwenye vilima na akawaita baadhi ya wanafunzi wake, hasa wale aliowataka wajiunge naye pale. 14 Akawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume. Aliwachagua ili waambatane pamoja naye, na kwamba aweze kuwatuma sehemu mbalimbali kuhubiri ujumbe wa neno la Mungu. 15 Pia aliwapa mamlaka ya kufukuza mashetani toka kwa watu. 16 Yafuatayo ni majina ya mitume kumi na wawili aliowateuwa Yesu:
Simoni ambaye Yesu alimwita Petro,
17 Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake (ambao wote Yesu aliwaita Boanergesi), yaani “wana wa ngurumo yenye radi”,
18 Andrea,
Filipo,
Bartholomayo,
Mathayo,
Thomaso,
Yakobo mwana wa Alfayo,
Thadayo,
Simoni Mzelote
19 na Yuda Iskariote,[a] ambaye ndiye aliyemsaliti Yesu.
Footnotes
- 3:19 Iskariote Yaweza kuwa “kutoka Kirioti”, mji kusini mwa Yuda.
Marko 3:13-19
Neno: Bibilia Takatifu
Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili
13 Yesu alipanda mlimani akawaita wale aliowataka, nao wakaja. 14 Akawachagua kumi na wawili wafuatane naye na awatume kuhubiri na 15 wawe na mamlaka ya kufukuza pepo. 16 Hawa ndio aliowachagua: Simoni, ambaye alimwita Petro, 17 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo ambao aliwaita Boanerge, yaani wana wa ngurumo; 18 Andrea; Filipo; Bartholomayo; Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Thadayo; Simoni, Mkanaani; na 19 Yuda
Read full chapter© 2017 Bible League International
Copyright © 1989 by Biblica