Luka 9:7-9
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Herode Achanganyikiwa Kuhusu Yesu
(Mt 14:1-12; Mk 6:14-29)
7 Herode, mtawala wa Galilaya alisikia mambo yote yaliyokuwa yanatokea. Alichanganyikiwa kwa sababu baadhi ya watu walisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu.” 8 Wengine walisema, “Eliya amekuja kwetu,” na baadhi ya watu wengine walisema “Mmoja wa manabii wa kale amefufuka kutoka kwa wafu”. 9 Herode alisema, “Nilimkata kichwa Yohana. Sasa, mtu huyu ninayesikia habari zake ni nani?” Herode aliendelea kutaka kumwona Yesu.
Read full chapter
Luka 9:7-9
Neno: Bibilia Takatifu
7 Habari zil imfikia Herode mtawala wa Galilaya kuhusu miujiza iliyokuwa iki fanyika, naye akafadhaika kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka!” 8 Wengine wakasema, “Ni Eliya ametutokea” na wengine kwamba, “Mmoja wa manabii wa kale amefufuka.” 9 Herode akasema, “Yohana nilimkata kichwa, ni nani huyu anayefanya maajabu haya ninayoambiwa?” Akajaribu sana amwone Yesu.
Read full chapter
Luke 9:7-9
New International Version
7 Now Herod(A) the tetrarch heard about all that was going on. And he was perplexed because some were saying that John(B) had been raised from the dead,(C) 8 others that Elijah had appeared,(D) and still others that one of the prophets of long ago had come back to life.(E) 9 But Herod said, “I beheaded John. Who, then, is this I hear such things about?” And he tried to see him.(F)
© 2017 Bible League International
Copyright © 1989 by Biblica
Holy Bible, New International Version®, NIV® Copyright ©1973, 1978, 1984, 2011 by Biblica, Inc.® Used by permission. All rights reserved worldwide.
NIV Reverse Interlinear Bible: English to Hebrew and English to Greek. Copyright © 2019 by Zondervan.
