1 Wakorintho 11:23-25
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
23 Mafundisho niliyowafundisha ni yale yale niliyopokea kutoka kwa Bwana, ya kwamba usiku ule ambao Bwana Yesu alikamatwa, aliuchukua mkate 24 na akashukuru. Kisha akaumega na kusema, “Huu ni mwili wangu; ni kwa ajili yenu. Uleni mkate huu kwa ajili ya kunikumbuka mimi.” 25 Kwa namna hiyo hiyo, baada ya wote kula, Yesu alichukua kikombe cha divai na akasema, “Divai hii inawakilisha agano jipya ambalo Mungu anafanya na watu wake, linaloanza kwa sadaka ya damu yangu. Kila mnywapo divai hii, fanyeni hivi kwa ajili ya kunikumbuka mimi.”
Read full chapter
1 Wakorintho 11:23-25
Neno: Bibilia Takatifu
Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, sitawasifu!
23 Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale maagizo niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alitwaa mkate, 24 naye akiisha kushukuru , akaumega, akasema, “Huu ndio mwili wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” 25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu.”
Read full chapter© 2017 Bible League International
Copyright © 1989 by Biblica