Add parallel Print Page Options

Bwana Mungu asema, “Mimi ni Alfa na Omega.[a] Mimi ndiye niliyepo, aliyekuwepo na anayekuja. Mimi ni Mwenye Uwezo Wote.” Mimi ni Yohana, mwamini mwenzenu. Tuko pamoja katika Yesu na tunashirikiana mambo haya: mateso, ufalme na uvumilivu wenye subira. Nilikuwa katika kisiwa cha Patmo[b] kwa sababu nimekuwa mwaminifu kwa ujumbe wa Mungu na kwa ajili ya kweli ya Yesu. 10 Siku ya Bwana, Roho Mtakatifu alinitawala. Nilisikia sauti kuu nyuma yangu iliyosikika kama tarumbeta.

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:8 Alfa na Omega Herufi ya kwanza na ya mwishi katika mfumo wa herufi wa Kiyunani, hapa inamaanisha “wa Kwanza na wa Mwisho”.
  2. 1:9 Patmo Kisiwa kidogo katika bahari ya Aegeani. Kisiwa hiki kiko karibu na pwani ya nchi ya Uturuki kama inavyojulikana siku za leo.