Add parallel Print Page Options

Ametufanya sisi kuwa ufalme wake na makuhani wanaomtumikia Mungu, Baba yake. Utukufu na nguvu viwe kwa Yesu milele na milele! Amina.

Tazama, Yesu anakuja pamoja na mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale waliomchoma.[a] Watu wote wa dunia watamwombolezea.[b] Ndiyo, hili litatokea! Amina.

Bwana Mungu asema, “Mimi ni Alfa na Omega.[c] Mimi ndiye niliyepo, aliyekuwepo na anayekuja. Mimi ni Mwenye Uwezo Wote.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:7 waliomchoma Yesu alipouawa, alichomwa mkuki ubavuni. Tazama Yh 19:34.
  2. 1:7 watamwombolezea Ama, “watajipiga vifuani mwao”. Usemi huu unatumika kuonesha huzuni na majonzi kwa yaliyomtokea pia hii ni ishara ya kuomboleza. Neno la Kiyunani lina maana ya kitendo zaidi ya kilio kwa sauti.
  3. 1:8 Alfa na Omega Herufi ya kwanza na ya mwishi katika mfumo wa herufi wa Kiyunani, hapa inamaanisha “wa Kwanza na wa Mwisho”.