17 Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mfu. Lakini yeye akaweka mkono wake wa kulia juu yangu akasema, “Usiogope. Mimi ni wa kwanza na wa mwisho. 18 Mimi ni Yeye aliye hai; nili kufa na tazama, mimi ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu.

Read full chapter

17 Nilipomwona nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Aliweka mkono wake wa kulia juu yangu na kusema, “Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa Mwisho. 18 Mimi ndiye ninayeishi. Nilikufa, lakini tazama, niko hai milele na milele! Na ninashikilia funguo za mauti na Kuzimu.

Read full chapter