26 Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa kumwamini Kristo. 27 Kwa maana nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo. 28 Hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanaume na mwanamke. Wote mmekuwa kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu. 29 Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wa uzao wa Ibrahimu na ni warithi wa ahadi aliyopewa na

Wana Wa Mungu

Nataka muelewe kwamba mrithi akiwa bado ni mtoto mdogo hana tofauti na mtumwa, ingawa mali yote ni yake. Kwa sababu anakuwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. Hali kadhalika na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa tunatawaliwa na kanuni za mazingira. Lakini wakati ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana we, ambaye alizaliwa na mwanamke chini ya sheria, ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.” Kwa hiyo, wewe sio mtumwa tena, bali ni mwana wa Mungu, na ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, basi wewe pia ni mrithi.

26 Hii ni kwa sababu ninyi nyote ni mali ya Kristo Yesu na ni watoto wa Mungu kwa njia ya imani. 27 Ndiyo, nyote mlibatizwa ili muunganike na Kristo. Hivyo sasa Kristo anawafunika kabisa kama kubadilisha nguo mpya kabisa. 28 Sasa, ndani ya Kristo haijalishi kama wewe u Myahudi au Myunani, mtumwa au huru, mwanaume au mwanamke. Wote mko sawa katika Kristo Yesu. 29 Na kwa vile ninyi ni wa Kristo, hivyo ninyi wazaliwa wa Ibrahamu. Ninyi ndiyo mtakaopokea baraka zote ambazo Mungu alimwahidi Ibrahimu.

Ninalolisema ni hili: Wakati mrithi wa vyote alivyomiliki baba yake bado ni mdogo, hana tofauti yo yote na mtumwa. Haijalishi kuwa anamiliki vitu vyote. Wakati wa utoto bado anapaswa kuwatii wale waliochaguliwa kumtunza. Lakini anapoufikia umri ambao baba yake ameuweka, anakuwa huru. Ndivyo ilivyo hata kwetu sisi. Mwanzoni tulikuwa kama watoto, tukiwa watumwa wa mamlaka za uovu[a] zinazoutawala ulimwengu huu wa sasa. Lakini wakati sahihi ulipofika, Mungu akamtuma Mwanaye, aliyezaliwa na mwanamke na akaishi chini ya sheria. Mungu alifanya hivi ili aweze kuwaweka huru wale waliokuwa chini ya sheria. Kusudi la Mungu lilikuwa kutuasili[b] sisi kama watoto wake.

Ninyi sasa ni watoto wa Mungu. Na ndiyo sababu Mungu amemtuma Roho wa Mwanaye mioyoni mwetu. Huyo Roho aliye ndani yetu hulia “Aba,[c] yaani Baba.” Sasa ninyi si watumwa kama mwanzo. Ni watoto wa Mungu, na mtapokea kila kitu ambacho Mungu aliwaahidi watoto wake. Hii yote ni kwa sababu ya yale ambayo Mungu amewatendea ninyi.

Footnotes

  1. 4:3 mamlaka za uovu Ina maana pia ya nguvu za giza.
  2. 4:5 kutuasili Ina maana ya kutufanya watoto wake na kutupa haki zote.
  3. 4:6 Aba Ni neno la Kiaramu lililotumiwa na watoto wa Kiyahudi kama jina la kuwaita baba zao.